January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Ulevi chanzo cha ajali nyingi’

Moja ya ajali mbaya za barabarani zilizotokea hivi karibuni

Spread the love

SERIKALI imesema, asilimia 74 ya ajali zinazotokea zinasababishwa na madeleva wengi kuendesha magari wakiwa wamelewa. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereila Ame Silima, alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kiwani, Abdalla Haji All (CUF).

Katika swali la msingi la mbunge huyo, alitaka kujua juhudi za serikali kuondoa tatizo la ajali ambalo linaonekana kuwa sugu.

Pia, alitaka kujua idadi ya Watanzania ambao wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabarani kuanzia Januari hadi Novemba mwaka jana.

Akijibu maswali hayo, Silima amesema kuwa asilimia kubwa ya ajali zinatokana na madereva wengi kujihusisha na ulevi wawapo barabarani.

Aidha, amesema kuwa kutokana na utafiti uliofanywa, unaonesha kuwa zipo sababu tatu za kusababisha kuwepo kwa vyanzo vya ajali.

Amezitaja kuwa ni kuwepo kwa makosa ya binadamu asilimia 74, ubovu wa vyombo vya usafiri asilimia 12 na hali duni ya miundombinu ya barabara inayochangia kwa asilimia 12.

Kuhusu idadi ya Watanzania waliopoteza maisha, Silima amesema kwa Januari hadi Novemba mwaka jana, ajali 2,887 zilitokea ambapo jumla ya Watanzania 3,528 wamepoteza maisha na 14,137 wamejeruhiwa.

Amesema kutokana na kuwepo kwa tatizo hilo, serikali inatumia askari wa usalama barabarani kuhakikisha wanatumia kamera ili kuthibiti vitendo hivyo.

error: Content is protected !!