July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ulaya, Marekani zapinga sheria ya mitandao Tanzania

Spread the love

MABALOZI wa Umoja wa Nchi za Ulaya na Marekani wamepinga sheria ya mitandao ya mwaka 2015 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madai kuwa hazizingatii haki za msingi za binadamu. Anaandika Josephat Isango … (endelea).

Tamko hilo la pamoja lilimetolewa na kukubaliwa na mabalozi wa nchi za Ubelgiji, Denmark, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Jamhuri ya Ireland ya Kaskazini, na Italia.

Wengine ni kutoka nchi za Hispania, Sweden, Uingereza, Norway, Uswisi pamoja na nchi za bara la America, Canada na Marekani.

Mabalozi hao wamesema kuwa utekelezaji wa sheria hiyo umeleta tafsiri hasi ya kisheria hivyo kubinya uhuru wa watanzania kwenye haki za kibinadamu.

Mabalozi hao wamesikitishwa na kitendo cha hivi karibuni cha serikali ya Tanzania kuwakamata viongozi wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC).

Serikali ya Tanzania ilitoa tamko maalum la kuanza utekelezaji rasmi wa sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 na sheria ya miamala ya kielektroniki ambayo imekuwa gumzo kubwa tokea kupitishwa sheria hizo huku wengi wakiiona kwamba itanyima uhuru wa kutoa na kupata habari

Tamko la kuanza utekelezaji rasmi wa sheria hizo mbili yaani ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 na sheria ya miamala ya kielektroniki ya mwaka 2015 lilitolewa na Wizara ya Mawasilaiano, Sayansi na Teknolojia kupitia waziri wake, Profesa Makame Mbarawa. Sheria hizo zilianza kutumika rasmi kuanzia Jumanne yaani Septemba mosi mwaka huu.

​Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa alisema hakuna ukweli wowote kwamba sheria hizi mbili zimeletwa ili kudhibiti uhuru wa mawasiliano kwa watanzania hususan wakati uchaguzi mkuu uliopita na kwamba wamejipanga ili kuhakikisha utekelezaji wake unakwenda kwa haki.

Kuanza kwa utekelezaji wa sheria hizi mbili za makosa ya mtandao ya mwaka 2015 na sheria ya miamala ya kielektroniki ya mwaka 2015 kunatokana na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha hatua hiyo hapo Aprili mosi mwaka huu. Sheria ambayo ilipingwa sana na asasi za kiraia na kambi ya Upinzani bungeni.

error: Content is protected !!