August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ulawiti wampeleka jela maisha

Spread the love

OMARY Hamisi mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Saalam amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka tisa ambaye ni ulemavu wa kuzungumza na kusikia, anaandika Aisha Amran.

Hukumu hiyo iliyotolewa na Flora Haule, Hakimu Mkazi, wa Mahakama ya wilaya ya Ilala imempata na hatia isiyotiliwa shaka, na kwa mujibu wa Haule, mahakama imeridhishwa na mashahidi tisa ukiwemo wa daktari na fomu Na 3 ya polisi (PF3) iliyotolewa mahakamani hapo kama kielelezo dhidi ya mshitakiwa huyo.

“mahakama imekukuta na hatia hivyo inakuhukumu kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na kosa la kumlawiti mvulana wa miaka tisa ambaye ni mlemavu wa kusikia na kuzungumza, ili iwe fundisho kwa jamii”. Alisikika Hakimu akisema

Katika ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, ilidaiwa kuwa mtoto huyo siku ya tukio alifika kwenye banda la kuonyeshea video ambalo linamilikiwa na Hamisi mida ya jioni, kwa ajili ya kuangalia video lakini Hamisi alimfukuza kutokana na kutokuwa na kiingilio.

Baada ya kumfukuza mtoto huyo aliondoka lakini baadae alirudi bila ya Hamisi kuwa na taarifa na kukaa ndani ya banda na kupitiwa usingizi uliosababisha abaki kwenye banda hilo peke yake hadi usiku.

Hamisi alitumia mwanya huo kumlawiti mtoto huyo kwenye jumba bovu lililopo jirani na ofisi yake hiyo.

Mashahidi waliieleza mahakama kuwa walisikia sauti ya mtu ambayo ilikuwa haisikiki vizuri akiomba msaada, ndipo waliposogea na kumkuta Hamis akitekeleza kitendo hicho huku akijua kuwa ni kosa kisheria.

Walidai kuwa hata walipomkaribia, Hamisi aliendelea kutekeleza kitendo hicho hadi walipolazimika kumpiga mateke. Hamisi amekiri kuwa siku hiyo mtoto huyo alifika kwenye banda lake.

Ester Kyara, ni Wakili wa serikali, ambaye aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wenye kufanya ukatili kwa watoto.

Katika utetezi wake Hamisi aliomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa madai kuwa ana familia inayomtegemea maombi ambayo yalitupiliwa mbali na mahakama hiyo na kuhukumiwa kifungo cha maisha.

Hamisi anadaiwa kutenda kosa hilo Agosti 26, 2014 eneo la Gongo la Mboto Dar es Salaam.

error: Content is protected !!