July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukwapuaji wa Escrow, Rutazibwa na Theophilo waburuzwa mahakamani

Wahusika wa sakata la Tegeta Escrow, kulia ni Mkurugenzi wa VIP Engineering, James Rugemalira na Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL, Harbinder Sing Sethi

Spread the love

SAKATA la akaunti ya Tegeta Escrow imechukua sura mpya, baada ya Mwanasheria wa RITA, Bw. Rutazibwa na Kaimu Kamishna wa Nishati na Petroli Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Theophilo Bwakea, kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu, anaripoti Erasto Stanslaus.

Watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani leo asubuhi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufuatia kuhusika na ukwapuaji wa fedha kutoka katika akaunti ya Escrow.

Hatua hiyo iliyochukuliwa na TAKUKURU inaweza kuwa mwanzo tu, kwani sakata hilo linawagusa wengi huku wengine wakiwa bado hawajachukuliwa hatua yoyote hadi sasa.

MwanaHALISI Online itakuletea habari hii kwa undani zaidi hivi punde.

error: Content is protected !!