Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Ukuta wa Simba, Yanga, kuathiriwa na swaumu ya Ramadhan?
Michezo

Ukuta wa Simba, Yanga, kuathiriwa na swaumu ya Ramadhan?

Saido Ntibanzokiza
Spread the love

 

KUELEKEA mchezo wa watani wa jadi (Simba na Yanga) kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara tutashuhudia baadhi ya wachezaji wanaocheza eneo la ulinzi kwa timu zote kuwa kwenye ibada ya Mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kuwa ni waumini wa dini ya kiislamu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo utapigwa siku ya Jumamosi tarehe 8 Mei, 2021, majira ya saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo imeangukia kwenye kipindi ambacho waumini wa dini ya kiislamu wapo kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na mchezo huo utakuwa kwenye Ramadhan ya 24.

Baadhi ya wachezaji wa timu hizo ambao kwa kiasi kikubwa wanacheza eneo la ulinzi, wataingia kwenye mchezo huo, huku wakiwa kwenye swaumu kutokana na mchezo huo kuanza majira ya saa 11.

Mohammed Hussein ‘Tshabalala’

Kwa upande wa wenyeji wa mchezo huo klabu ya Simba walinzi wao, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein na Mlinda mlango wao, Aishi Manula watakuwa wakicheza mchezo huo huku wakiwa kwenye mfungo.

Wengine kutoka ndani ya kikosi cha Simba, ambao huenda wakapata nafasi ya kuanza kwenye mchezo huo huku wakiwa kwenye mfungo ni kiungo wao mkabaji, Mzamiru Yassin pamoja na kinara wao wa mabao, Meddy Kagere.

Wageni wa mchezo huo timu ya Yanga, huenda ikawa na idadi kubwa ya wachezaji wa eneo la ulinzi watakaocheza wakiwa kwenye mfungo, ambao ni mabeki wao wa pembeni, Shomari kibwana na Adeyum Salehe pamoja na walinzi wa kati Abdallah Shaibu (Ninja), Bakari Nondo na Lamine Moro.

Wachezaji wengine ambao wanapewa nafasi kubwa kuanza kwenye mchezo huo, ambao pia watakuwa kwenye ibada hiyo ya Ramadhan ni kiungo wao, Feisal Salum, Haruna Niyonzima na Saido Ntibanzokiza.

Timu hizo mbili zinakutana huku zikiwa kileleni kwenye msimamo wa Ligi, ambapo Simba ipo kwenye nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 61 na michezo 25, huku Yanga ikiwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 mara baada ya kucheza michezo 27.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!