July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ukuta kiboko, Marekani yajihami

Spread the love

SALAMU za maandamano na mikutano ya hadhara chini ya operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta (Ukuta) nchini, zatia hofu Marekani, anaandika Charles William.

Raia wa nchi hiyo wanaoishi Tanzania wametakiwa kuchukua tahadhari kutokana na maandalizi yanayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuratibu maandamano na mikutano hiyo licha ya kuwepo kwa vitisho vya Jeshi la Polisi na viongozi wa serikali nchini.

Kwa sasa, kuna vuta nikuvute kuhusu kufanyika kwa maandamano na mikutano hiyo hasa baada ya Rais John Magufuli kutangaza kuzuia mikutano hiyo isipokuwa kwa viongozi husika wa jimbo kauli ambayo inakwenda kinyume na uhuru wa kidemokrasia nchini.

Wakati maandamano na mikutano yakipangwa kuanza Septemba Mosi mwaka huu, ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, umetahadharisha raia wake na kuwataka kuwa makini pamoja na kutojichanganya pale itakapofanyika.

Operesheni ya kupinga kile kinachoitwa ‘udikteta’ unaotajwa kuchipuka kwa kasi nchini, Freeman Mbowe kwa niapa ya Kamati Kuu ya chama hicho, Julai mwaka huu alitangaza kuanza kufanyika kwa operesheni hiyo (Ukuta).

Mbowe ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa pia ndiye kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upunzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika taarifa ya Ubalozi wa Marekani kwa raia hao, imewataka kuepuka kujichanganya katika mikusanyiko ya maandamano ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

“Ingawa maandamano hayo yametangazwa na viongozi wa vyama vya upinzani kuwa yatakuwa ya amani lakini yanaweza kuibua vurugu kutokana na mvutano uliopo,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza zaidi kuwa, “ingawa raia wa Marekani hapa nchini wamekuwa siyo walengwa katika maandamano yaliyopita.

“…lakini tunawatahadharisha kuepuka mikusanyiko ya watu na maeneo ambayo maandamano hayo yatafanyikia,” imeeleza taarifa hiyo.

Pamoja na kuwepo kwa vitisho vinavyofanywa na Jeshi la Polisi, viongozi wa Ukawa wamegoma kurudi nyuma ambapo wanaendelea kushawishi wanachama wao pia ‘wapenda haki’ kujitokeza kwenye mikutano na maandamano hayo.

error: Content is protected !!