Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Ukusanyaji mapato: Majaliwa atoa maagizo vigogo Tamisemi
Habari Mchanganyiko

Ukusanyaji mapato: Majaliwa atoa maagizo vigogo Tamisemi

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa na viongozi wengine wa wizara hiyo wahakikishe suala la ukusanyaji mapato kwenye Mikoa, Halmashauri na Mamlaka za Serikali za Mitaa linapewa kipaumbele ili kuongeza mapato ya Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

“Ajenda ya ukusanyaji mapato iwe ya kudumu ili yaongezeke hadi kufikia shilingi trilioni 2 kutoka makadirio ya sasa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo Halmashauri zimekadiria kukusanya mapato ya ndani ya shilingi trilioni 1.01 ikilinganishwa na shilingi bilioni 863.85 zilizoidhinishwa kwa mwaka 2021/2022,” alisema.

Majaliwa alitoa wito huo jana Jumanne, tarehe 31 Mei 2022 alipokutana na Waziri wa Tamisemi, Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na Wakurugenzi na Wakuu wa taasisi za wizara hiyo kwenye kikao alichokiitisha jijini Dodoma ili kuwakumbusha wajibu wao.

“Nimekuja kwenye ziara ya kawaida ya kiutendaji ili kuzungumza na viongozi wakuu wa wizara na wakuu wa idara. Ni lazima ujitambue wewe ni nani hapa kwenye wizara, unatakiwa kufanya nini, mpango kazi wako ukoje na je ni wako peke yako ama unahitaji watu wengine ili uweze kuutekeleza,” amesema.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anataka kuona Watanzania wanafikiwa na huduma. Ni lazima tujiulize, je huduma hizo zinafika kwa wananchi kwa wakati. Watanzania wanaitegemea Tamisemi kuanzia ngazi ya mkoa, wilaya, halmashauri, kata vijiji hadi vitongoji. Kwa hiyo, tunapaswa kuhakikisha hiyo chain inafanya kazi,” alisema.

Alisema watumishi hao wanapaswa kutambua kwamba bila uaminifu, uadilifu na uwajibikaji hawawezi kufanikiwa lakini pia wanapaswa kusimamia mambo hayo matatu hadi ngazi za chini

Aliwapongeza viongozi na watendaji wa wizara kwa kufanikiwa kuongeza hati safi kwenye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) katika kipindi cha mwaka 2019/2020 na 2020/2021.

“Taarifa ya CAG kuhusu Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2020/2021 imebainisha Halmashauri 178 sawa na asilimia 96 zimepata hati safi, Halmashauri sita sawa na asilimia tatu zimepata hati zenye shaka na Halmashauri moja sawa na asilimia moja imepata hati mbaya.”

Waziri Mkuu alisema matokeo ya ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha 2020/2021 yanaonesha mwenendo mzuri wa aina ya hati za ukaguzi zilizotolewa ikilinganishwa na ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha wa 2019/2020 ambapo Halmashauri zilizopata hati safi zilikuwa 124 sawa na asilimia 67, Halmashauri zilizopata hati zenye shaka zilikuwa 52 sawa na asilimia 29 na Halmashauri zilizopata hati mbaya zilikuwa nane sawa na asilimia nne.

“Mwaka huu hati mbaya zimepungua kutoka nane hadi moja, kwa hiyo kama leo tumefikia asimilia 96 tuna uwezo wa kufikia asilimia 100, kutafuta ile mbaya na zenye mashaka sita zikaondoka.”

Aliitaka menejimenti ya wizara hiyo iwe na ubunifu, iongeze matumizi ya TEHAMA ili kuongeza mapato ya Serikali, Wakuu wa Idara wagawe majukumu kwa wasadizi wao na wakurugenzi wawe na vikao vya mara kwa mara na wasaidizi wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!