Tuesday , 23 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Ukusanyaji damu wabadilisha mwelekeo
Afya

Ukusanyaji damu wabadilisha mwelekeo

Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu katika Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Dk. Avelina Mgasa
Spread the love

 

MPANGO wa Taifa wa Damu Salama umebadilisha mwelekeo wake wa kuigeukia jamii ili kukusanya damu kwa ajiri ya kukabiliana na changamoto ya kutegemea wanafunzi wa shule za sekondari iliokuwa ikiwatumia wakati wote. Anaripoti Glory Massamu, TUDARCo … (endelea).

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Taifa ya Ukusanyaji Damu iliyoanza tarehe 20 Septemba 2021, Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu katika Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Dk. Avelina Mgasa amesema kauli mbiu ya kampeni za mwaka huu ni Changia Damu Kuokoa Wanaoleta Uhai Duniani.

Dk. Mgasa amesema hivi sasa wanaweka mkazo kwa jamii kujitolea damu kwa hiari kwani Mpango wa Taifa wa Damu Salama haujaweza kufikia lengo la kukusanya chupa za damu zinazokithi mahitaji ya nchi.

Ripoti ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama imeonesha kwa kipindi cha mwaka 2019/2020 kwa kushirikiana na timu za halmashauri wameweza kukusanya chupa za damu 312,714 zilikusanywa ambazo ni sawa na asilimia 57 ya mahitaji, amesema.

Dk. Mgasa amesema shirika la afya Dunniani (WHO) linaelekeza kila nchi mwanachama kukusanya damu asilimia moja ya wakazi wake au chupa 10 kwa kila wananchi 1,000 ili kujitosheleza na mahitaji ya damu salama wakati wote.

Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu katika Mpango wa Taifa wa Damu Salama, amesema kwa takwimu za mwaka 2019/2020 Tanzania tumefikia chupa 6 kwa kila wananchi 1,000.

Akizungumzia changamoto za kupata wachangiaji wa damu, amezitaja ni pamoja na wanafunzi wanaosoma na hata wanaomaliza shule za sekondari kuwa na umri mdogo kwani sharia inawataka watu wenye umri wa miaka 18 hadi 65.

Asilimia 80 ya damu inayokusanywa nchini inakusanywa kutoka kwa wanafunzi na vijana wanapokuwa shule za sekondari na vyuoni ambao wanamaliza wakiwa na umri mdogo hivyo hawapati fursa ya kuchangia damu wakiwa shuleni na wakirudi kwenye jamii huacha kuchangia, anasema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!