Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Ukraine yakomboa jiji la Kyiv kutoka Urusi
Kimataifa

Ukraine yakomboa jiji la Kyiv kutoka Urusi

Spread the love

 

WAKATI mazungumzo ya kusitisha vita kati ya Urusi na Ukraine yakiendelea kwa kusuasua, Serikali ya Ukraine imesema imechukua udhibiti wa eneo zima la Kyiv baada ya wanajeshi wa Urusi kurudi nyuma kutoka katika baadhi ya miji muhimu karibu na mji huo mkuu.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa kuna hofu ya kutegwa mabomu ya ardhini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Ganna Maliar ameandika kwenye ukurasa wa Facebook hapo jana tarehe 2 Aprili kuwa miji ya Irpin, Bucha, Gostomel na eneo zima la Kyiv imekombolewa kutoka kwa mvamizi.

Miji hiyo ilikuwa imeharibiwa vibaya kutokana na mapigano hayo na raia wengi waliuawa.

Meya wa miji hiyo amesema watu 280 walizikwa katika kaburi la pamoja katika mji wa Bucha na miili mignine ikiwa imesambaa kwenye mji huo huku mamlaka zikisema karibu watu 200 waliuawa katika mji wa Irpin tangu Urusi ilipoivamia Ukraine.

Ukraine imesema askari wa Urusi wanaondoka kwenye maeneo ya kaskazini na wanaonekana kujielekeza zaidi upande wa mashariki na kusini mwa Ukraine.

Kwenye ujumbe wake wa video kwa taifa jana usiku, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema wanajeshi wa Ukraine wanayakomboa maeneo ya karibu na Kyiv na Cherhiniv hivyo hawatawaruhusu Warusi kuondoka bila mapambano.

Aidha, Rais huyo kwa mara nyingine ameomba msaada wa zana za kisasa za kivita kutoka kwa nchi za magharibi kama vile ndege na mifumo ya kuyaharibu makombora.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!