September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukraine yadai imetengwa vita dhidi ya Urusi, ICC kuingilia kati 

Spread the love

 

RAIS wa Ukraine, Volodomyr Zelenskky, amesema dunia imewaacha peke yake katika mapambano ya kivita dhidi ya Urusi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Rais Zelenskky ametoa kilio hicho leo Ijumaa, tarehe 25 Februari 2022, siku moja baada ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin,  kutangaza operesheni ya kivita katika mikoa mwili ya mashariki mwa Ukraine, inayodhibitiwa na waasi , ambao wametangaza kijitenga na Taifa hilo.

Kiongozi huyo wa Ukraine amedai kuwa, leo amezungumza na viongozi 27 wa Ulaya,ili kuomba msaada lakini hakuna aliyejibu kutokana na kuwa na hofu.

Hata hivyo, Rais Zelenskky amesema licha ya kukosa msaada watapambana kulipigania Taifa lao, huku akiwataka wanaume kuanzia umri wa miaka 18 hadi 50 kujitokeza mstari wa mbele kuikomboa nchi yao.

“Tumeachwa peke yetu kulilinda Taifa letu,  nani yuko tayari kupigana na sisi? Sioni mtu yeyote kila mmoja anaogopa. Leo nimeongea na viongozi 27 wa Ulaya, niliwauliza moja kwa moja kila mmoja alikuwa anaogopa, hakuna majibu. Lakini hatutaogopa, hatuogopi kwa chochote. Hatutaogopa kulilinda Taifa letu hatuogopi Urusi,” amesema Rais Zelenskky.

Rais wa Ukraine, Volodomyr Zelenskky

Rais Zelenskky amesema vikwazo vilivyojaribu kuwekwa na mataifa ya nje dhidi ya Urusi, havitoshi kuliwajibisha Taifa hilo, dhidi ya uamuzi wake wa kuivamia Ukraine, huku akituhumi vikosi vyake vinashambulia maeneo ya kiraia.

Hadi sasa, raia wa Ukraine,  takribani 140 wanaripotiwa kufariki dunia.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), Karim Khan, amesema mahakama yake itachunguza vita ya Urusi na Ukraine, ili kubaini kama kuna uhalifu wa kivita kwa ajili ya kuchukia hatua.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN, Antonio Gutteres, kupitia taarifa aliyoichapisha kwenyw ukurasa wake wa Twitter,  ameionya Urusi iache mara moja mapigano hayo, akisema kitendo hicho ni kinyume na mkataba wa umoja huo.

Aidha, Gutteres ameyataka mashirika yanayotoa msaada wa huduma za kibinadamu, kuanza operesheni zake nchini Ukraine ili kuokoa maisha ya raia wasiokuwa na hatia.

error: Content is protected !!