January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukosefu wa chakula wachangia utoro mashuleni

Wanafunzi wa shule ya msingi

Spread the love

UKOSEFU  wa Chakula sheleni hususan zile zinazomilikiwa na serikali umetajwa kuwa chanzo kikubwa kinasababisha wanafunzi kutoroka mashuleni na kwenda kujitafutia chakula hali inayoathiri taaluma na maendeleo ya elimu nchini. Anaandika Ferdinand Shayo, Arusha … (endelea)

Mwanakijiji wa kijiji cha Arkata, Kipara Ngine amesema kuwa watoto wengi wamekua wakitoroka shuleni kwa kukosa chakula hivyo kupelekea idadi ndogo ya mahudhurio  mashuleni.

Kipara ameiasa saerikali kwa kushirikiana na mashirika binafsi pamoja na wazazi kuhakikisha upatikanaji wa chakula  katika sahule ya msingi Arkata iliyopo wilaya ya Monduli mkoani hapa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Kipi Alarosi amesema kuwa licha ya changamoto ya utoro bado shule hiyo inakabiliwa na uchakavu wa majengo na upungufu wa madarasa hivyo ameiomba jamii na wapenda maendeleo wajitokeze kuiwezesha shule hiyo iweze kufanya vizuri kitaaluma.

“Shule haina madirisha na majengo yamechakaa mvua ikinyesha inaingia mpaka darasani watoto hawasomi vizuri hata kipindi cha jua vumbi linajaa darasani “ Amesema Alarosi.

Mkurugenzi wa Shirika la wafugaji Monduli Pastoralist Development  (MPDI), Erasto Sanare  amesema kuwa baada ya kupokea ombi la shule hiyo watatua fedha za ukarabati wa  madarasa ya shule hiyo ili kuwajengea watoto mazingira bora.

Amesema  mwamko wa jamii ya wafugaji katika masomo umekua kwa kiasi kikubwa  mashirika na watu binafsi yakijitoa kusaidia kutatua changamoto zao ili watoto wa wafugaji wapate elimu bora.

error: Content is protected !!