May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ukerewe kupata maji safi Julai 30

Spread the love

ZAIDI ya Sh. 20 bilioni zimetumika kwenye ujenzi wa mradi mkubwa wa maji safi, katika Mji wa Nansio wilayani Ukerewe, Mwanza uliokuwa unakabiliwa na tatizo sugu la maji tangu taifa kupata Uhuru mwaka 1964, anaandika Moses Mseti.

Mradi mwingine ni wa maji taka na taka ngumu utakaogharimu Sh. 2.159 bilioni, huku taka hizo zikizalishwa kwa ajili ya umeme (bio gas) wa nyumbani pamoja na matumizi mengine ya kijamii wilayani humo.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa ziara ya kukagua miradi hiyo miwili inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira (Mwauwasa) mkoa wa Mwanza, Mkandarasi wa miradi hiyo, Mhandisi, Samwel Getanda, amesema kuwa wanatarajia kuikabidhi miradi hiyo Julai 30 mwaka huu.

Amesema kuwa miradi hiyo ingekuwa imekwisha kabidhiwa tangu mwanzoni mwa mwezi huu lakini tatizo lililosababisha zoezi kukwama ni kutokana na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha nchini.

“Asilimia 98 ya miradi hii tayari tumekwisha imaliza na ikifika mwishoni mwa mwezi huu, tutakuwa tumemaliza hivyo itakuwa tayari kukabidhi kwa mamlaka husika na kama mnavyoona wenyewe kila kitu tumekwisha maliza,” amesema Getanda.

Edward Joseph, Meneja wa Mwauwasa wilayani humo amesema kuwa, Wananchi wa Ukerewe walikuwa wanakabiliwa na tatizo la maji safi pamoja na usafi wa mazingira kwa muda mrefu kitendo ambacho kilihatarisha maisha yao.

Amesema wilaya hiyo yenye watu zaidi ya 70, 000, mpaka hivi sasa tayari watu wengi wameanza kuomba kuunganishiwa maji huku akidai kuwa mradi wa maji safi utakuwa unazalisha zaidi ya lita 35,000 kwa siku.

Gogadi Mgwatu, Mhandisi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira (Mwauwasa), mkoani hapa amesema kuwa miradi hiyo inayotekelezwa katika nchi tano za Jumuiya ya Afrika mashariki, nchini inatekelezwa kwenye wilaya tatu.

Mgwatu alizitaja Wilaya hizo kuwa ni Geita, Sengerema na Nansio wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, baada ya vigezo na masharti ya jumuiya hiyo, iliyotaka Wilaya zinazokabiliwa na tatizo la maji safi na maji taka.

error: Content is protected !!