July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukeketaji ni mateso – TAMWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa. Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Valeria Msoka

Spread the love

WANAWAKE waliowengi Kaskazini mwa Tanzania, wamefanyiwa vitendo vya ukeketaji, maarufu kama “tohara ya wanawake.”

Ripoti ya kitafiti ya Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), imetaja sababu kadhaa zinazosababisha kuwapo ukeketaji.

Miongoni mwa sababu hizo, ni kuwapo vitisho dhidi ya wasichana.

Mkoani Mara, kabila la Wakurya ndilo linaloongoza katika vitendo vya ukeketaji. Wakurya wanasisitiza, “mwanamke asiyekeketwa, hastahili kuolewa.” Vitendo vya ukeketaji vimekuwa vikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Kwa mfano, mwaka 2004 ukeketa ulikuwa asilimia 38.1; mwaka 2010 ukeketaji uliongezeka hadi kufikia asilimia 39.9. Ongezeko hili ni sawa na asilimia1.8.

Kuongezeka kwa vitendo hivyo, kunaashiria kuwa jitihada za kukomesha ukatili huo, bado hazijafanikiwa.

Kati ya Novemba na Desemba ya kila mwaka, ni msimu wa ukeketaji huko Tarime, ambako maelfu ya wasichana huwa wanakeketwa. Baada ya shughuli hiyo kukamilika, hufuata sherehe za kuwapongeza na kuwatoa ndani kama ishara ya ukuaji.

Hiki ni kipindi cha nderemo. Ngoma ya jadi aina ya Ritungu nayo huzidi kupata umaarufu kwenye msimu huu.

Jesca Edward, ni miongoni mwa wanawake walionusurika kukeketawa akiwa mdogo. Hii ni baada ya kukimbia kutoka kwa wazazi wake.

Akiwa binti wa kwanza katika familia ya watoto wanane, Jesca alilazimika kukimbia nyumbani kwao, Serengeti mkoani Mara na kwenda kuishi kwa mama yake mdogo, mkoani Morogoro.

Jesca ambaye kwa sasa ana watoto watatu anasema, ilikuwa vigumu kwake kuhama nyumbani, lakini alilazimika kufanya hivyo ili kuinusuru na ukeketaji.

“Nilikimbia nyumbani, saa 10 alfajiri. Wakati huo nilikuwa darasa la sita. Baada ya kufika Morogoro, nashukuru niliendelea na masomo yangu ya msingi na baadaye nikafanikiwa kufika sekondari,” anaeleza.

Anasema kwa sasa, amefungua taasisi yake binafsi inayopinga ukatili wa kijinsia na wamekuwa wakizunguka maeneo mbalimbali kupinga mila hiyo.

Lakini ukimsikiliza Jesca na kujipa muda wa kutafiti angalau kidogo, utaweza kugundua haraka kwamba serikali haijawekeza vya kutosha katika mapambano ya kukomesha ukeketaji.

Kwa mfano, Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), kimeeleza katika utafiti wake katika Wilaya ya Singida Vijijini, kwamba asilimia 95 ya wanawake wanaojifungulia hospitalini mwaka 2012, wamepata tohara.

TAMWA inasema, pamoja na mila na desturi, umaskini nao unazisukuma familia nyingi kukeketa watoto wao kwa lengo la kujiongezea kipato.

Mathalani, mkoani Mara, kabila la Wakurya lenye ukwasi mkubwa wameweka viwango vya aina ya mwanamke wanayetaka kumuoa. Katika kabila hili, “mwanamke hastahili kuolewa.”

error: Content is protected !!