August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukawa yaanza kuibadili taswira ya Kinondoni

Spread the love

MANISPAA ya Kinondoni na Kampuni GAFF ya nchini Ujerumani wameingia mkataba wa kushauri na kubuni ujenzi wa miundombinu na miradi ya maendeleo (DMDP) kwenye manispaa hiyo, anaandika Faki Sosi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kabla ya kusaini mkataba huo Boniface Jacob, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo amesema kuwa, mshauri huyo mwelekezi wa mradi huo utakaoghalimu Sh. 50 bilioni, atafanya utafiti wa jinsi ya kujenga miundomibinu ya barabara kwenye manspaa hiyo. Mtandao wa MwanaHalisi Online umeshuhudia uingiaji mkataba huo.

Jacob ambaye ni Diwani wa Kata ya Ubungo (Chadema) amesema kuwa, fedha zimetolewa na Benki ya Dunia ili kudhamini miradi hiyo na kwamba, miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa barabara 13 ambazo zitadumu kwa zaidi ya miaka 20.

Akitaja baadhi ya barabara amesema ni Barabara ya Maji ya Chumvi hadi Korogwe, Mburahati hadi NIT, Manzese Darajani hadi Urafiki.

Jacob amesema kuwa, kwa mara ya kwanza manispaa hiyo itaujengea Mto wa Ng’ombe na Mto Msimbazi kwa teknolojia ya kisisasa ili kuzuia maafa.

“Mradi huo utahusisha ujenzi wa Mto Msimbazi kuanzia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi Hananasifu ambapo manispaa itawalipa fidia wakazi walio karibu na mto huo ndani ya mita 30,”amesema Jacob.

Thorste Sertz, Maneja wa Kampuni GAFF Tawi la Tanzania amesema kuwa, atahakikisha anabuni miradi itakayoifanya kinondoni kuwa na miundombinu mizuri.

error: Content is protected !!