July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukawa wazua hofu bungeni, Polisi wajipanga kuwakabiri

Spread the love

UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umezua hofu kubwa bungeni kutokana na hali ya kutangaza msimamo wao wa kutokukubaliana na Rais John Magufuli kulihutubia Bunge. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Jana umoja huo ulitangaza rasmi kwamba umemwandikia spika barua ya kuhoji uhalali wa Rais kulihutubua bunge wakati uchaguzi wa Zanzibar umefutwa na kulifanya taifa la Zanzibar kutokuwa na rais.

Hali hiyo imeifanya serikali kuwa na hofu kubwa ambayo inaonekana kuwatesa viongozi wa CCM siku ya leo iwapo msimamo wao utaendelea kuwa huo.

Ili kuonesha kuwa hofu ni kubwa leo kuanzia asubuhi, maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma hususani katika maeneo ya bunge kuwepo kwa magari ya polisi ya maji ya kuwasha.

Mbali na magari ya polisi yenye maji ya kuwasha yakiwa yameegeshwa katika maeneo mbalimbali ya bunge, magari mengine ya jeshi la polisi yalionekana kurandaranda huku yakiwa yamesheheni askari.

Hali hiyo imetafsiriwa na baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma kuwa ni njia pekee ya kuwatishia watanzania kutokana na tangazo la Ukawa la kutomtaka Rais John Magufuli kulihutubia Bunge.

Baadhi ya viongozi mbalimbali ambao walizungumza na MwanaHALISI Online walieleza kwamba jeshi la polisi limekuwa likitumia nguvu nyingi kuhakikisha wananchi wanatishiwa jambo ambalo ni usumbufu mkubwa na kuwanyima haki ya kudai haki yao.

Mmoja wa makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema kitendo cha serikali kutumia jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa ni kinyume na utawala bora bora.

Naye mmoja wa viongozi wa bodaboda wa kituo cha Swaswa, Salumu Mohamed Swaswa, amesema umefika wakati wa watanzania kuonesha hisia zao katika kufanya maamuzi.

Mohammed, amesema ni wajibu wa wananchi kuhakikisha wanafanya maamuzi ambayo yataonesha wazi utashi wao, jambo la kujua ni kwamba maandamano ni haki ya msingi kwa watanzania pale wanapoona kwamba hawatendewi haki.

Amesema Waziri yeyeto ambaye angepatikana jambo pekee ni kuhakikisha utendaji wa kazi kwa maslahi ya wananchi bila kujiangalia wenyewe.

error: Content is protected !!