Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ukawa wazidi kumsulubu Ndugai, wamsusia futari
Habari za Siasa

Ukawa wazidi kumsulubu Ndugai, wamsusia futari

Spread the love

WABUNGE wa kambi ya upinzani bungeni, jana waliamua kumsusia futari, Spika wa Bunge, Job Ndugai, anaandika Mwandishi Wetu.

Taarifa kutoka kiongozi mmoja mwandamizi kutoka ndani ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) zinasema, uamuzi wa wabunge hao kususia futari umetokana na madai kuwa Spika amekuwa akiendesha Bunge kwa upendeleo.

Hoja ya kususia futari iliwasilisha kwenye kikao kilichofanyika jana kabla ya Bunge kukutana kupitisha bajeti.

“Tulikutana jana na tukakubaliana kwa kauli moja kususia futari hiyo. Hatuwezi kushirikiana na watu wanaotubagua waziwazi,” ameeleza mbunge mmoja wa UKawa aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina.

Habari zinasema, mbali na mkakati huo, Ukawa umejipanga kukabiliana na serikali hasa kutokana na kauli kuwa “wabunge waliopinga bajeti wanyimwe fedha za maendeleo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

error: Content is protected !!