July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukawa wawashushia lawama wakurugenzi

Spread the love

WAGOMBEA ubunge katika majimbo mbalimbali katika kanda ya ziwa kupitia vyama vya upinzani wamelalamikia kitendo walichofanyiwa na wakurugenzi kwa kuwanyima ushindi makusudi. Anaandika Dany Tibason, Bukombe … (endelea).

Wabunge hao wakizungumza na MwanaHALISI Online kwa nyakati tofauti wamesema kwamba wakurugenzi wengi walifanya makusudi kuhakikisha wagombea hao wa upinzani washindwa.

Mmoja wa wagombea ambao walikuwa wakigombea katika jimbo la Bukombe, Prof. Kulikoyela Kahigi amesema wameanza kulalamikia jambo hilo kwa muda mrefu lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Amesema kumekuwepo kwa shinikizo kwa wakurugenzi wa halmashauri zote za kanda ya ziwa kuhakikisha wabunge wa upinzani wanashindwa.

Naye aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum Conchester Rwamlaza amesema CCM imetumia fedha nyingi kuhakikisha inadhoofisha upinzani zaidi.

Naye aliyekuwa mbunge wa Biharamulo Magharibi, Dk. Antony Mbassa amesema kimsingi CCM imetumia nguvu nyingi ya kifedha kwa ajili ya kuonga na kuwatishia wananchi wasiipigie kura wapinzani.

Hata hivyo wamesema kuwa pamoja na kuwepo kwa vitisho vya CCM kwa wananchi watahakikisha wanaendelea kujenga chama ili kuwaelimisha wananchi wajue haki zao.

error: Content is protected !!