June 24, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ukawa wavuruga tena bungeni

Spread the love

LEO wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wametibua taratibu za Bunge kwa mara nyingine, anaandika Faki Sosi.

Wametoka nje baada ya Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge kuongoza Bunge hilo, hatua hiyo ni mwendelezo wa kupinga kuhudhuria vikao hivyo kuongozwa na kiongozi huyo.

Hata hivyo, mtindo wa leo wa Ukawa umekuwa tofauti na siku zote hususani katika mavazi. Ukawa wameingia bungeni wote wakiwa wamevaa mavazi meusi kuashiria kuwa, Bunge lipo kwenye msiba mzito.

Kwa muda mrefu sasa, wabunge wa upinzani wamekuwa wakilalamikia Dk. Tulia kuminya upinzani na kukibeba chama tawala-Chama Cha Mapinduzi (CCM).

error: Content is protected !!