June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

UKAWA watua mzigo, wagawa majimbo 253

Spread the love

VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), vimetangaza mgawanyo wa majimbo 253 kati ya majimbo 265 ya uchaguzi Tanzania Bara huku majimbo 12 yakibaki kwenye majadiliano. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Kwa upande wa Zanzibar majimbo yote ya uchaguzi wamekabidhiwa Chama cha Wananchi (CUF) isipokuwa Jimbo la Mkwajuni ambalo wamepewa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwepo kwa makubaliano ya pamoja miongoni mwa vyama vinavyounda umoja huo. UKAWA unaundwa na vyama vinne vya siasa ambavyo ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi pamoja na NLD.

Taarifa ya mgawanyo huo imetolewa leo mchana jijini Dar es Salaam na Makaimu Katibu Wakuu wa vyama hivyo; Sheweji Mketo (CUF), Nderakindo Kessy (NCCR – Mageuzi), Masudi Makujunga (NLD) na John Mnyika (Chadema) na taarifa hiyo kusainiwa kwa mapoja.

Mketo amesema vigezo vilivyotumika katika mgawanyo huo ni chama kilichoongoza katika matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 katika jimbo husika, matokeo ya udiwani katika kata za majimbo.

Pia matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2014, mtandao wa vyama katika eneo husika, mila na desturi katika eneo husika, ubora wa mgombea na maridhiano ya vyama vyote.

“Hii ndiyo taarifa ya kwanza rasmi kuhusu mgawanyo wa majimbo. Tunasisitiza wanachama wetu wanapaswa kutambua kwamba, taarifa hii haihusiani na mchakato wa kuwapata wagombea wa udiwani. Tulishatoa mwongozo kuhusu upatikanaji wa wagombea ngazi ya udiwani,” amesema Mketo.

Ufuatao ni mgawanyo wa majimbo katika kila mkoa Tanzania Bara;-

Mkoa wa Mara

Kwenye mkoa huu majimbo yote tisa wamekabidhiwa Chadema. Majimbo hayo ni Rorya, Tarime Mjini, Tarime Vijijini, Musoma Vijijini, Butiama, Bunda Mjini, Mwibara, Musoma Mjini na Bunda Vijijini.

Mkoa wa Simiyu

Chadema wamegawiwa Jimbo la Bariadi, Maswa Magharibi, Maswa Mashariki, Kisesa, Meatu, Itilima ambapo Busega limekwenda kwa CUF.

Mkoa wa Shinyanga

Majimbo ya Mkoa wa Shinyanga ambayo ni Msalala, Kahama Mjini, Kahama Vijijini, Shinyanga Mjini, Kishapu na Ushetu yamekwenda Chadema.

Mkoa wa Mwanza

Jimbo la Ukerewe, Magu, Nyamagana, Buchosa, Sengerema, , Ilemela, Misungwi yamekabidhiwa Chadema kuhu Jimbo la Kwimba na Sumve wakikabidhiwa CUF.

Mkoa wa Geita

Bukombe, Busanda, Nyang’wale, Chato na Mbogwe yamekwenda Chadema.

Mkoa wa Kagera

Jimbo la Karagwe, Kyerwa, Bukoba Mjini, Muleba Kaskazini, Muleba Kusini, Biharamulo yamekwenda Chadema ambapo Jimbo la Ngara na Nkenge yamekwenda NCCR-Mageuzi na Bukoba Vijijini limechukuliwa na CUF.

Mkoa wa Mbeya

Katika Mkoa wa Mbeya Jimbo la Lupa, Songwe, Mbeya Mjini, Kyela, Rungwe, Busekelo, Mbozi Mashariki, Momba, Mbeya Vijijini, Tunduma na Viwawa yamekwenda Chadema huku Ileje likikabidhiwa kwa NCCR.

Mkoa wa Iringa

Jimbo la Ismani, Kalenga, Mufindi Kaskazini, Iringa Mjini, Kilolo na Mafinga Mjini yamekabidhiwa kwa Chadema ambapo Jimbo la Mufindi Kusini linapiganiwa na NCCR-Mageuzi.

Mkoa wa Dar es Salaam

Jimbo la Ubungo, Kawe, Ukonga, Ilala na Kibamba ni Chadema huku Kinondoni, Temeke, na Mbagala ikielekezwa kwa CUF.

Mkoa wa Njombe

Njombe Kaskazini, Lupembe, Wanging’ombe, Makete, Ludewa na Makambako yamekwenda Chadema.

Mkoa wa Rukwa

Jimbo la Mkasi Kusini, Kwela, Mkasi Kaskazini, Sumbawanga Mjini na Kalambo ni Chadema.

Mkoa wa Tanga

Handeni Mjini, Handeni Vijijini, Pangani, Tanga Mjini, Bumbuli, Mlalo, Lushoto na Mkinga ambapo Korogwe, Muheza, Kilindi na Korogwe Vijijini ni Chadema.

Mkoa wa Kilimanjaro

Jimbo la Rombo, Same Magharibi, Same Mashariki, Moshi Vijijini, Siha, Moshi Mjini na Hai ni Chadema huku Vunjo ikienda kwa NCCR.

Mkoa wa Arusha

Jimbo la Arumeru Mashariki, Arumeru Magharibi, Arusha Mjini, Longido, Monduli, Karatu na Ngorongoro ni Chadema.

Mkoa wa Manyara

Jimbo la Simanjiro, Mbulu Vijijini, Hanang, Babati Mjini, Babati Vijijini, Kiteto na Mbulu Mjini ni Chadema.

Mkoa wa Pwani

Jimbo la Bagamoyo, Kisarawe, Mkuranga, Rufiji Utete, Mafia, Rufiji na Kibiti ambapo Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini na Chalinze ni Chadema.

Mkoa wa Morogoro

Jimbo la Kilosa na Morogoro Kusini Mashariki (CUF) ambapo Mikumi, Morogoro Kusini, Kilombero, Mlimba, Mvomero, Ulanga Magharibi, Ulanga Mashariki na Morogoro Mjini ni Chadema.

Mkoa wa Dodoma

Jimbo la Kondoa Mjini, Kondoa Vijijini na Chema ni CUF; Jimbo la Kibakwe na Mtera ni NCCR-Mgeuzi huku Jimbo la Kogwa, Dodoma Mjini, Bahi na Chilonwa yakiwa ni ya Chadema.

Mkoa wa Singida

Jimbo la Iramba Magharibi, Iramba Mashariki, Singida Kaskazini, Singida Mashariki, Singida Magharibi, Manyoni Magharibi na Manyoni Mashariki ni Chadema.

Mkoa wa Tabora

Jimbo la Bukene, Nzega Vijijini, Igalula, Tabora Kaskazini, Kaliua na Tabora Mjini ni CUF ambapo Jimbo la Nzega Mjini, Igunga, Urambo, Ulyankulu, Sikonge na Manonga ni Chadema.

Mkoa wa Katavi

Jimbo la Mpanda Mjini, Mpanda Vijijini, Katavi, Nsimbo na Kavuu ni ya Chadema.

Mkoa wa Kigoma

Buyungu, Mhambwe, Kasulu Mjini, Kasulu Vijijini, Kigoma Kusini, Manyovu (NCCR-Mageuzi) na Kigoma Kaskazini pia Kigoma Mjini ni Chadema.

Mkoa wa Ruvuma

Jimbo la Tunduru Kaskazini, Namtumbo na Tunduru Kusini ni CUF ambapo Mbiga Mjini ni NCCR-Mageuzi. Jimbo la Madaba, Songea Mjini, Mbinga Mashariki/Mbinga, Mbinga Maghribi/Nyasa na Peramilo ni Chadema.

Mkoa wa Mtwara

Jimbo la Newala Mjini, Newala Vijijini, Tandahimba, Mtwara Vijijini, Nanyamba na Nanyumbu ni CUF ambapo Jimbo la Lulindi, Masasi na Ndanda ni NLD.

Mkoa wa Lindi

Jimbo la Mtama, Kilwa Kaskazini, Kilwa Kusini, Lindi Mjini, Ruangwa, Nachingwea, Liwale na Mchinga ni CUF.

error: Content is protected !!