January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukawa watoa onyo kali Uchaguzi wa Meya Kinondoni

Spread the love

MBUNGE wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea kwa niaba ya  vyama vinavyounda  Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ametoa  onyo kwa wabunge na madiwani wa  Zanzibar walio kuja kuongeza idadi ya madiwani wa CCM waondoke haraka kwani uchaguzi  wa Umeya na madiwani wa Tanzania Bara si la Muungano. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam katika ofisi za (Chadema)  amesema, kwa mujibu wa Katiba na sheria za serikali za mitaa hakuna kipengele  kinachozungumzia juu ya madiwani au wabunge wa Zanzibar wanaweza kuja Tanzania Bara  kushiriki katika uchaguzi.

“Serikali za mitaa sio suala la Muungano kwa hivyo haliwahusu Zanzibar inamuundo wake wa serikali za mitaa, pia kasoro nyingine kubwa inayowakosesha haki ya kushiriki katika mchakato huu,  hao waliokuja wote sio wakazi wa Dar es Salam sifa ya diwani ni lazima awe mkazi wa eneo hilo”. Amesema Kubenea

Ameongeza kuwa, ujaji wa madiwani na wabunge kuja kushiriki katika uapishaji wa madiwani na uchaguzi wa meya ulikuwa ni mpango wa CCM baada ya kuona idadi yao ni ndogo.

“Hao wabunge walioletwa  katika fomu zao bungeni walijaza kuwa ni wakazi wa Zanzibar na hata malipo yao ya nauli za kuwatoa makwao hadi bungeni hulipwa kutokea Zanzibar na sio Dar es Salaam hata fomu zao za viapo waliapa hivyo.

Amesema  ukiyachambua yote hayo unakuta bado hawana haki ya kupiga kura huku, ni vema warudi kwao wakamalize migogoro yao na watuachie ngoma yetu tuicheze wenyewe CCM na UKAWA.

“ Walituibia kura za Rais wetu Edward Lowassa na sasa wanataka pia watuibie kwenye uchaguzi wa meya wa Wilaya  na Meya wa Jiji hatutakubali tuko macho na tupo radhi hata huo muungano uvunjike kama serikali na taasisi zake itaendeleza upuuzi huu.

Naye Mbunge wa      Jimbo la Ukonga  Mwita Waitara amesema, kitendo kinachofanywa na CCM ni kutaka kuvuruga uchaguzi wa mameya baada ya kugundua kuwa ushindi ni wa Ukawa kwa kuwa wamekosa madiwani katika majimbo yote isipokuwa la Segerea na ndio maana hawakupeleka mamruki wa kuongezewa.

Akitolea mfano, Jimbo la Ilala ambapo Chadema wanamadiwani  na viti maalumu 28, CUF 7 jumla ni ni 35 ambapo CCM wanajumla ya madiwani na viti maalumu 27 hali inayo wapa  wakati mgumu.

“Wanataka kulazimisha kupata Meya wa Jiji kitu ambacho hatutakubali kwani jumla yetu ni 91 na wao wapo 71 ukiwaondoa mamluki  20 ambao wameletwa ili kuja kujazia tuonekane tupo sawa. Lakini kihalali kama tukiwaondoa hao mamluki ushindi wetu kulingana na  idadi yetua”. Anesema Waitala

Pia wamemtaka Rais John Magufuli kuendesha nchi kwa kufuata misingi ya utawala bora,   hivyo wamemtaka atende haki na kuyazuia mambo ambayo yanakiashiria cha uvunjifu wa amani nchini.

error: Content is protected !!