Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ukawa watangaza vita na NEC uchaguzi wabunge
Habari za SiasaTangulizi

Ukawa watangaza vita na NEC uchaguzi wabunge

Spread the love

VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuahirisha uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Januari 13, 2018 vinginevyo havitashiriki, anaandika Faki Sosi.

Vyama hivyo ni Chadema, CUF, Chauma, NLD na NCCR-Mageuzi.

Akizungumza kwa niaba ya Ukawa leo Jumatatu Desemba 11 ,2017, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema vyama hivyo havitashiriki uchaguzi kwa sababu ya kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata 43 uliofanyika Novemba 26,2017.

Mbowe amesema uchaguzi huo uligeuka kuwa uwanja wa vita badala ya kuwa jukwaa la kuchagua viongozi.

“Ndiyo maana tunaiomba Serikali kuahirisha uchaguzi ili wadau wajadili kasoro zilizojitokeza,” amesema.

Amesema majadiliano ya wadau yatasaidia kuondoa kasoro zilizojitokeza, hivyo kuwa na uchaguzi ulio huru na haki.
Mbowe amesema iwapo Serikali kupitia NEC itakataa kuahirisha uchaguzi wao hawatashiriki.

“Hatuwezi kushiriki uchaguzi wakati tumefungwa mikono, hii ni sawa na timu ya mpira kwenda kwenye mashindano bila kufanya mazoezi,” amesema.

Mbowe amesema wakati vyama vya upinzani vikizuiwa kufanya mikutano ya hadhara, chama tawala kinafanya mikutano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!