August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukawa washinda Umeya Ubungo, CCM hoi

Spread the love

VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimetwaa Manispaa ya Ubungo leo, anaandika Pendo Omary.

Boniface Jacob (Chadema) ameshinda kiti cha Umeya wa manispaa hiyo jijini Dar es Salaam baada ya kupata kura 16 dhidi ya kura mbili za Yusuph Yenga, mgombea wa CCM.

Kwenye uchaguzi huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa manispaa hiyo uliopo Kibamba, Ramadhan Kwangaya, mgombea unaibu Meya kutoka CUF amepata kura 15 dhidi ya Kassim Lema wa CCM aliyepata kura tatu.

Meya Jacob baada ya ushindi amesema kuwa, atashirikiana na watendaji wote katika kuhakikisha analeta maendeleo kwenye manispaa hiyo mpya iliyogawanywa kutoka katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Katika Manispaa ya Kinondoni Jacob alikuwa Meya na sasa ni Meya wa Manispaa ya Ubungo baada ya uchaguzi wa leo.

“Nitaongoza kwa utatu mtakakatifu yaani watumishi, wanasiasa na wananchi. Nitasimamia mgawanyo wa Ubungo na Kinondoni na maswala yote yaliyopangwa katika bajeti inayoendelea, mikopo ya kina mama na vijana,” amesema.

error: Content is protected !!