January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

UKAWA walia rafu za CCM, wamchana Masaburi

Spread the love

UMOJA wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umelalamika rafu wanazofanyiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku zikifumbiwa macho na vyombo vya dola, pamoja na Tume ya Uchaguzi. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Matukio yaliyojitokeza hivi karibuni kwa nyakati tofauti dhidi yao, yakiwemo ya vijana kutumwa kufanya fujo katika ofisi zao, kuchana mabango ya mgombea wao, pamoja na vijana wa chama hicho kukamatwa na Polisi bila sababu.

Umoja huo wa UKAWA unaundwa na vyama vinne ambavyo ni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), NCCR-Mageuzi, Chama Cha Wananchi (CUF) na NLD.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo katika ofisi za muda za UKAWA jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema mambo yanayofanywa na CCM yakuchochea waumini na viongozi wao, wananchi kwa wananchi, majeshi na vyombo vya usalama ni siasa zilizopitwa na wakati

Mbatia ambae pia ni Mwenyekiti mwenza wa UKAWA, ameelezea tukio lililotokea juzi na kusema kuwa ni tukio la kinyama ambalo linaweza kuharibu amani ya wananchi na kuleta mapigano.

Mwenyekiti mwenza huyo amemtaja kiongozi wa CCM ambae alihusika kuandaa tukio la vijana kufanya fujo kwa kutumia jina la Chadema kuwa ni Didas Masaburi ambae ni mgombea ubunge katika Jimbo la Ubungo.

Masaburi ambae pia alikuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam alishiriki kuwatuma vijana hao kwa kuwapatia fulana ya Chadema, skafu, na pesa kama malipo ya kwenda kufanya fujo.

“Alichokifanya Masuburi ni kiashiria tosha kwamba hawezi kushindwa kuwatuma watu hata na mapanga kuja kufanya fujo. Kumbukeni mapigano ya Kenya yaliyotokea mwaka 2007 damu ilimwagika kwa sababu ya uchochezi wa kisiasa,” amesema Mbatia.

Amedai kwa matukio hayo yote yaliyotokea yakiwemo ya kuchanwa kwa mabango UKAWA wanashangazwa na ukimya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi hadi sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

“Tumeshayapeleka matukio yote pamoja na ushahidi wa kutosha katika vyombo husika tunasubiri matokeo na haki itendeke. Pia niwaombe wanasiasa kutotumia kinyume vyombo vya dola kwani si watumishi wa chama kimoja bali wapo kwaajili ya Watanzania wote,” amesema.

Kuhusu kampeni Mbatia amesema: “Zinaendelea vizuri na mapokezi ya wananchi ni makubwa sana tofauti na CCM na bado tunasimamia agenda yetu kubwa ni kuleta katiba mpya iliyopendekezwa na wananchi.”

error: Content is protected !!