July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge wa UKAWA wakomaa, kuzuia miswada nje ya Bunge

Spread the love

WABUNGE wa Upinzani ambao juzi na jana wametimuliwa bungeni kwa madai kuwa ya kufanya fujo bungeni na kudharau mamlaka ya Spika wamesema wataendelea na harakati zao za kupinga miswada ya madini na gesi ambayo inajadiliwa kwa sasa. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Mbali na hilo Wabunge hao wamesema Spika, Anne Makinda amekuwa kiongozi pekee wa kukanyaga na kudharau kanuni za bunge kwa kuendesha bunge kwa kusikiliza mashinikizo kutoka nje ya bunge.

Licha ya kukanyaga kanuni za bunge imeelezwa kuwa Spika amelidhalilisha bunge kwa kushindwa kusimamia kanuni za bunge na badala yake anaendesha bunge kwa mashinikizo ya Rais Jakaya Kikwete ambaye amelazimisha miswada mibovu kupelekwa bungeni kwa hati ya dharura.

Akizungumza kwa niaba ya wezake Mnadhimu wa Kambi rasimi ya upinzania Bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amesema si kweli kuwa wametoka bungeni kwa ajili ya fujo bali waliondolea bungeni kwa ajili ya kutetea maslahi ya watanzania na vizazi vijavyo.

Lissu alisema kitendo cha kuwafukuza wabunge wa upinzani bungeni ni dalili tosha ambazo zilikusudiwa na mafisadi wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Rais Kikwete ili kuuza nchi kwa mikataba ya wazi.

Kiongozi huyo alisema mikataba ya mafuta na gesi uwasilishwaji wake bungeni umekiuka kanuni za bunge kwani mswada huo umetolewa tangazo la serikali mara moja ambapo inatakiwa utangazwe katika gazeti hilo mara mbili na wabunge wote wapate nakara za miswada husika.

Mnadhimu huyo alienda mbali zaidi kwa kusema iwapo mikataba hiyo itapitishwa na bunge ni wazi kuwa rais ajaye atakuwa amefungwa mikono kwani mikataba hiyo haina tofauti na kuiuza nchi kama ilivyofanyika mwaka 1997 na 1998 ambapo bunge kwa hati ya dharura ilipitisha mikataba ya madini ambapo kwa sasa taifa alinufaiki na madini hayo.

“Ikumbukwe kuwa kwa miaka ya 1997/98 kwa mtindo huu ambao wanaufanya kwa mikata ya mafuta na gesi bunge lilipelekewa mswada wa madini ambayo kwa sasa yanaonekana kuwepo nchini na sasa madini hayo siyo mali yetu.

“Hata hivi kama watapitishwa mswada huu ni sawa na kwamba nchi itakuwa imeuzwa na gesi yake kwa sababu hakuna mswada mbovu wenye sheria mbovu na za ovyo kama ilivyo kwa mswada huu wa gesi.

“Nataka niwaambie ndugu waandishi sisi tunajuiliza ni kwanini kuna uharaka kiasi hili sasa sababu ni hii , wakati tulipokuwa katika kamati ya maofisa wa serikali kutoka Wizara ya Nishati na Madini, walisema serikali imesema nilazima mswada huo upitishwe ili mwezi Septemba serikali inapokwenda kuomba fedha katika Serikali ya Marekani na China waweze kupatiwa fedha.

“Na kama mswada huo utashindikana na bila kupata sheria ni wazi hizo fedha haziwezi kutolewa na mkumbuke tunaelekea katika kipindi cha uchaguzi,” amesema Lissu.

Kwa upande wake Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) alisema pamoja na wao kuondolewa ndani ya ukumbi wa bunge lakini bado wanaendelea kujipanga kuhakikisha mswada huo haupiti.

Alisema pamoja na kutumia wingi wao na Spika kuvunja kanuni za wazi wazi lakini wataendelea na vikao kwa ajili ya kuhakikisha mswada huo haupiti.

Alisema kuna bunge kubwa zaidi na lenye mamlaka ambalo lipo kwa wananchi na mahakama kubwa zaidi ambayo ni wananchi ambao wanaweza kutoa maamuzi makubwa zaidi kuliko mahakama au maamuzi ya Spika ndani ya bunge.

Kwa upande wake Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini  na Mbunge wa Gondo (CUF), Kharifa Suleimani  Kharifa walisema kauli iliyotolewa na kamati ya ya haki maadili na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Brigedia Jeneral, Hasani Ngwilizi kwamba wamejutia makosa yao ni kauli ya kipumbavu.

Selasini amesema kauli hiyo ni ya kipuuzi na kipumbavu wala yeye hajajutia makosa hayo kwani hajafanya kosa lolote ndani ya bunge na badala yake ametimiza wajibu wa kutetea maslahi ya taifa.

“Sasa mimi nina haki ya kuingia bungeni kesho (leo) sasa wataona nitakachokifanya wasifikilie sisi ni watu wa kutetea maovu ambayo yanafanywa na serikali kwa kulindwa na kiti cha Spika wanafanya hivyo kwa lengo la kutaka kutugawa,” amesema.

error: Content is protected !!