July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukawa wagomea matokeo ya NEC

Spread the love

UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusitisha kutangaza matokeo ya urais yanayoendelea kutangazwa kwani si matokeo halisi bali yamejaa ulaghai na wizi “ni feki”. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam katika ofisi za Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) iliyopo Kawe, wakati viongozi wa umoja huo wakizungumzia matokeo yanayotanagzwa na NEC yanatofautiana na idadi ya wapiga kura.

Mgombea urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa amesema, tangu uchaguzi ulipoanza Ukawa waliziona kasoro nyingi na walipotoa taarifa NEC iliwapuuza na kuendelea kutangaza matokeo.

Lowassa amesema NEC ipo mfukoni mwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani imekuwa ikipendelea jinsi ya kutangaza matokeo ambapo imekuwa ikiyatangaza maeneo ambayo CCM imeshinda.

“Kabla ya vijana wetu 191 wa kukusanya matokeo kutoka mikoa mbalimbali kuvamiwa na kukamatwa juzi na Jeshi la Polisi pasipo makosa yoyote tulikuwa tayari tuna asilimia 67 ya ushindi. CCM, NEC na Jeshi la polisi wana njama ya kutukosesha ushindi kwa kuvuruga mitambo yetu.

Kutokana na makosa hayo yote yanayofanyika na bila kuchukuliwa hatua yoyote mimi pamoja na mgombea mwenza Juma Duni Haji tunatangaza kutokubaliana na matokeo haya, hivyo NEC isiendelee kuyatangaza kwani ni batili la si hivyo tutachukua hatua kali tunataka kura zirudiwe kuhesabiwa bila kutumia mashine zao feki,” amesema Lowassa.

Kwa upande wake, Duni amesema NEC na serikali ilipania kuuvuruga uchaguzi huu kwa makusudi kwani kura feki zimekuwa zikikamatwa mara kwa mara lakini NEC ipo kimya kama haioni kinachoendelea.

“Tangu mwanzo mimi niliona hilo, NEC iliongeza kura hewa milioni tisa na nilipolisema ikasema naingilia kazi yake matokeo yake ndio haya, wizi wa kura nje nje hadi wananchi wanagundua,” amesema Duni.

Duni akitolea mfano wa majimbo ambapo Mgombea urais wa CCM aliongezewa kura amesema, Chalinze aliongezewa kura 1000, Mkuranga kura 100 na maeneo mengine mengi. Ambapo amesema tatizo hilo pia hata Zanzibar limetokea.

Naye Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amesema ameluwa akishangazwa na utendaji wa NEC kwani umekuwa hauko makini na hivyo kusababisha wizi wa kura kushamiri hata kabla ya siku ya upigaji kura kufika.

Akitolea mfano wa maroli yaliyokamatwa mikoa mbalimbali ikiwemo Tunduma Mbeya, ambapo ndani yake kulikuwa na maboksi ya kura feki, lakini NEC ilikuwa kimya hivyo ni wazi kwamba inashirikiana na wezi au imeshindwa kazi yake.

Sumaye amesema: “Ni vema NEC iangalie jambo hili tena kwa makini ili nchi hii isije kuingia kwenye machafuko baada ya wananchi kumkosa rais wanayemtaka badala yake wanachaguliwa.”

Wakati huohuo, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Francis Mbatia amesema Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza kufuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika kwa kile walichokiita uchaguzi haukuwa wa haki.

“Ilichofanya ZEC ndicho kinachoendelea hapa Bara kwa sasa. Iyo ni wazi kuwa CCM, serikali na ZEC imeshirikiana kuuvunja uchaguzi huo kwa kuwa mgombea urais wetu kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif ameshinda wanaona aibu kutangaza matokeo,” amesema Mbatia.

error: Content is protected !!