July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘UKAWA tumejipanga kuipeleka nchi pazuri’

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akipokea mundu kutoka kwa mmoja wazee wa chama hicho wa Dar es Salaam, Mwinyijuma Said Mahugila, wakimsimika kuwa Chifu wa Kizaramo, wakati wa Kongamano la Baraza la Wazee wa Chadema

Spread the love

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamejipanga kuitoa nchi kwenye umaskini uliokithiri uliosababisha na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakichukua dola. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Aidha, wamewataka wazee kusimamia kidete kuwasaidia vijana katika zoezi la uandikishaji kupitia mfumo wa kielektroniki (BVR) kwa kuwa wizi wa kura unaanzia hapo na kuwataka wananchi kuhakikisha wanajiandikisha.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam leo na Katibu Mkuu wa Chadema Dk.Wilbroad Slaa wakati akihutubia Baraza la wazee kujadili mustabali ya taifa kuelekea uchaguzi mkuu.

Amesema wazee ndio chimbuko la nchi wanapaswa kusikilizwa na kupewa kipaumbele na kusema kuwa kinachotokea bungeni  sasa ni vita kati ya ubadhirifu na ufisadi ndio maana hata wa upinzani wametimuliwa bungeni huku Spika Anna Makinda akitengua kanuni kwa makusudi ili kukilinda chama tawala.

Amesema katika ufisadi chama hicho kinawatumia  wazee kuwatoa kutoka mikoa mbalimbali na kuwalipa posho ya shilingi 5,000  ili wahudhurie kwa wingi katika mikutano yao hawana mada za kujenga wanazo za kusambaratisha wananchi.

Dk. Wilbroad Slaa akihutubia kwenye Kongamano la Wazee wa Chadema
Dk. Wilbroad Slaa akihutubia kwenye Kongamano la Wazee wa Chadema

“Chadema haina uwezo wa kumlipa kila mmoja anayehudhuria katika vikao tuna uwezo wa kuwakusanya na kuwalisha vitu vizuri vya kujenga nchi na si kubomoa”amesemaDk.Slaa.

Akizungumzia baada ya kuchukua dola kupitia UKAWA wataleta mabadiliko katika nchi kwa kuboresha miundombinu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha nyumba  za nyasi zinaondoka nchini kwa kuwa Tanzania ina rasilimali za kutosha.

Amesema serikali kupitia CCM wamekuwa wakijisifu kuwa wamewaletea maendeleo wananchi ilihali kuwa maendeleo hayo yameletwa nawananchi wenyewe kupitia kodi zao.

Kupitia mkutano huo Dk.Slaa alivishwa kanzu,koti huku akikabidhiwa shoka kama Chifu wa  wazee mkoa wa Dar es Salaam na kubatizwa jina la kizaramo la Mwinyikambi.

error: Content is protected !!