June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ukawa ‘kufukua makaburi’

Boniface Jacob, Meya wa Manispaa ya Ubungo

Spread the love

HATUA ya serikali kuendesha zoezi la bomoabomoa katika maeneo ya Kata za Kiluvya, Mbezi na Msigani inapaswa kufuatiliwa, anaandika Pendo Omary.

Ni kauli ya Boniface Jacob, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, jijini Dae es Salaam aliyoitoa jana baada ya kutangazwa kushinda kwenye uchaguzi wa meya.

Jacob amesema manispaa hiyo ina kila sababu ya kufuatilia bomoabomoa inayoendelea kata hizo ili kujiridhisha kama ni njama za serikali dhidi ya maeneo yaliyoipa kura vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ama la!

Vyama vinavyounda umoja huo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha NCCR-Mageuzi na NLD ambapo kwenye kata hiyo vipo Chadema na CUF pekee.

Jacob ametoa kauli hiyo baada ya Humphrey Sambo, Diwani wa Kata ya Mbezi (Chadema) kuwasilisha malalamiko ya wananchi wa maeneo hayo kubomolewa bila kufuata utaratibu wa kisheria.

Sambo amesema “mwanzo tuliambiwa bomoabomoa itakuwa ndani ya mita 120 kutoka barabarani, lakini kilichofanyika sio sahihi.

“Katika zoezi hili wananchi wamenyanyaswa na kudhalilishwa. Utaratibu wa kisheria haukufuatwa.”

“Kuhusu bomoabomoa inayoendelea Jimbo la Ubungo, mimi na madiwani wangu tutakaa chini tutaitathimini kama ni kweli ya maendeleo au imetumwa. Huenda ni bomoabomoa ya kufanya kwa kuwa, huku kuna wapinzani,” amesema Jacob na kuongeza;

“Hatutakuwa tayari kuona wananchi wetu wakionewa kwa sababu za siasa.”

Pia Sambo alipomtaka John Kayombo, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuchukua hatua za haraka kwa kuwatembelea wananchi walioathirika na bomoabomoa hiyo ili kuangalia ili kujua msaada gani wa haraka unaoweza kutolewa, Kayombo alijibu “kwa sasa zoezi limesitishwa.”

“Tayari nimeagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kusitisha bomoabomoa ili kupata nafasi ya kujiridhisha na madai yanayotolewa na wananchi,” amesema Kayombo.

error: Content is protected !!