Monday , 26 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa UKAWA kuanikwa siri ya ushindi ya Unaibu Meya
Habari za SiasaTangulizi

UKAWA kuanikwa siri ya ushindi ya Unaibu Meya

Frederick Sumaye, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani (katikati) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani
Spread the love

MWENYEKITI wa Chadema, Kanda ya Pwani, Fredrick Sumaye, atakutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, muda wowote wiki hii. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema, mkutano huo utakaofanyika ndani ya wiki hii katika makao makuu ya Chadema, Kanda ya Pwani, Sumaye ataongoza na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka Chama cha Wananchi (CUF).

Miongoni mwa viongozi hao, ni Julius Mtatiro, mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya taifa, Shaweji Mketo, naibu mkurugenzi wa uchaguzi, Riziki Shaari Ngwali, mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa na Kafana Mussa Kafana, naibu meya wa jiji la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyama vyote viwili – CUF na Chadema – mkutano kati ya viongozi hao na waandishi wa habari, umelenga kueleza “mikakati ya vyama hivyo, katika kukabiliana na CCM.”

“Mwenyekiti wetu wa Kanda, Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, atakuja kueleza uzoefu wake wa kuwa CCM kwa miaka zaidi ya 40. Atakuja kueleza mipango ya vyama vyetu kukabiliana na utawala huu,” anaeleza Saed Kubenea, makamu mwenyekiti wa kanda ya Pwani.

Kubenea ambaye pia ni mbunge wa Ubungo (Chadema) amesema, mbali na hilo, mkutano huo utatumika kueleza mikakati ya Ukawa ya kuendesha halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.

Jiji la Dar es Salaam, tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa 25 Oktoba 2015, liko chini ya vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

“Mkutano wa leo unalenga pia kueleza waandishi wa habari, siri ya mafanikio ya UKAWA katika kuliendesha jiji hili,” ameeleza Kubenea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!