August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukatili washamiri Mwanza

ACP Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza

Spread the love

IMEELEZWA kuwa, makosa ya ukatili dhidi ya binadamu katika Mkoa wa Mwanza yameongezeka hadi kufikia matukio 749 kwa mwaka mpaka sasa huu kutoka matukio 447 ya mwaka jana, anaandika Moses Mseti.

Hayo yameelezwa jana na Robert Mwita, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Kitengo cha Dawati la Jinsia, wakati wa mafunzo ya mwanamabadiliko yalioandaliwa na Shirika la Kutetea Wanawake (Kivulini) Mkoa wa Mwanza.

Mwita amesema kuwa, matukio hayo ya ukatili yameripotiwa polisi kutokana na mwamko na elimu inayotolewa na mashirika mbalimbali hususan Kivulini wanaotoka elimu kwenye jamii kuhusu umhimu wa kuyaripoti matukio hayo.

Amesema kuwa, awali wananchi walikuwa wakishindwa kuripoti matukio hayo ya kikatili kutokana na ukosefu wa elimu ikilinganishwa katika kipindi hiki ambacho wameelimika.

Makosa hayo ni pamoja na kutorosha wananfunzi, kutelekeza jamii, wanafunzi kupewa mimba, kabaka, kalawitiwa, kakatisha wanafunzi masomo na mauaji.

Hata hivyo, amesema kuwa makosa ambayo yameonekana kuripotiwa kwa kiasi kikubwa katika dawati lake ni pamoja na kutorosha wanafunzi, wanafunzi kupewa mimba, kubaka na kutelekeza familia.

“Kuna changamoto nyingi ambazo polisi tunalalamikiwa ikiwa ni pamoja na rushwa zinazodaiwa chukuliwa na baadhi ya polisi na suala hili tutakabiliana nalo ili kuondoa kasumba hii na kuondoa wasi wasi kwa wananchi,” amesema Mwita.

Yassin Ally, Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Wananwake (Kivulini) amesema kuwa, asilimia 96 ya wanafunzi wanaopewa mimba shuleni huozeshwa na walimu wakuu wa shule na wazazi wa wanafunzi hao kwa kushirikiana na watendaji wa serikali za mitaa na kata.

Ally amesema kuwa, walimu pamoja na wazazi wa wanafunzi hao hufanya mpango wa kuwaozesha wanafunzi kutokana na kuendekeza vitendo vya rushwa na kwamba, asilimia 75 ndoa hizo baadaye hutelekezwa.

Mafunzo hayo ya siku moja yamewakutanisha wadau tofauti wakiwamo, polisi kitengo cha jinsia, walimu, watendaji wa kata, wanaharakati, wanamabadiliko na maafisa maendeleo ya jamii kutoka mkoani hapa.

 

error: Content is protected !!