May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukata wateka mdahalo urais TLS

Spread the love

 

CHANGAMOTO ya upungufu wa fedha inayokikumba Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), imeteka mdahalo wa wagombea urais wa chama hicho, uliofanyika leo Jumatano, tarehe 27 Aprili 2022, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Waliojitosa kugombea urais wa TLS katika uchaguzi mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mei, 2022, ni Profesa Edward Hosea, Jeremiah Mtobesya na Harold Sungusia.

Akizungumza katika mdahalo huo, Sungusia amesema jambo lililomsukuma kugombea nafasi hiyo ni ukata wa fedha ulioikumba TLS kiasi cha kupeleka kushindwa kulipa wafanyakazi wake mishahara kwa miezi mitano.

“Jambo lililoniasababisha niingie kwenye kinmyang’anyiro cha urais TLS , ni baada ya kusikia eti chama changu kilikaa miezi mitano bila kulipa wafanyakazi wake mishahara kwa sababu ya kukosa pesa. Inakuwaje chama kikubwa chenye wanachama 10,000 kikose pesa ifikie mahali ya kufunga chapter zake,” amesema Sungusia.

Kwa upande wake Mtobesya, amedai chanzo cha ukata wa fedha TLS imesababishwa na uongozi uliokuwepo kupunguza vyanzo vya mapato bila ya kutafuta njia mbadala ya kufidia upungufu wa fedha.

“Hapa katikati chama kimetetereka kwenye masuala ya kifedha na mbaya zaidi wameshindwa kutekeleza baadhi ya majukumu. Nimefuatilia nimeona baada ya bajeti kutungwa wakategemea mapato ya chanzo fulani. Uongozi uliokuja waliondoa baadhi ya vyanzo vya mapato bila ya njia mbadala ya kuziba pengo,”amedia Mtobesya na kuongeza:

“Baada ya muda mchache chama kikawa hakina hela, na ukweli uelezwe chama chetu chanzo cha mapato muhimu ni tozo. Nikiingia nitaimarisha mapato ya chama.”

Naye Prof. Hoseah, amesema katika uongozi wake amefanikiwa kuishawishi Mahakama Kuu ya Tanzania kurejesha Sh. 450 milioni, zinazotolewa na mawakili kama ada.

“Tumerudisha Sh. 450 milioni ambazo tangu uhuru tulikuwa tukilipa mahakama kama ada, hatujawahi kurudishiwa. Kwa uongozi wangu zimetengwa Sh. 450 milioni, sasa jamani mnataka tufanyeje? Mimi sio wa blab la, ni wa vitendo nimetekeleza,” amesema Dk. Hoseah na kuongeza:

“Nimeongea na Serikali imekubali kutenga Sh. 1.4 Bil. kwa ajili ya ruzuku katika zoezi la utoaji msaada wa kisheria kwa wananchi sababu TLS inatekeleza majukumu ya umma, wale ambao mnasema kwamba hii ni rushwa, Serikali haiwezi kuionga TLS, hii hela ni ya wavuja jasho.”

error: Content is protected !!