August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukata wamuondoa Pluijm Yanga

Hans van Pluijm

Spread the love

KLABU ya Yanga imesitisha mkataba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi, Hans Van Der Pluijm kutokana na klabu hiyo kutokuwa na uwezo wa kuendelea kumlipa, anaandika Erasto Masalu.

Pluijm alikuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo kwa misimu miwili kabla ya kupandishwa na kuwa mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo, lakini sasa amefunguliwa milango ya kuondoka.

“Nimepewa barua asubuhi hii na Yanga juu ya mkataba wangu kuwa umesitishwa. Walichokisema ni kuwa klabu kwa sasa ina Ukata na hawana uwezo wa kuendelea kunilipa,” amesema Pluijm.

“Kwa sasa nipo huru kujiunga na klabu yeyote itakayoonyesha nia na mimi basi nitafanya nao kazi.” Alisisitiza Pluijm.

error: Content is protected !!