January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukarimu wa watanzania utawagharimu

Wananchi wanaoishi mazingira duni

Spread the love

NAKUMBUKA  ile hadithi ya watoto wa simba na watoto wa swala  walivyokutana kwenye bonde la pori na kucheza pamoja  na kufurahiana bila kujuana jua lilipozama kila wakaelekea makwao na kuwakuta wazazi wao na kushindwa kujizuia furaha waliyokua nayo. Anaandika Ferdinand Shayo, Arusha … (endelea).

Kwa  kukutana na marafiki wapya watoto wa swala  wakawa wa kwanza kumsimulia mama yao, akawaambia walikua wanacheza na hatari kwani wangeweza kuuawa na kufanywa kitoweo basi wakaambiwa kesho hao marafiki watoto wa simba wakija muwaambie kuwa kama mama yenu hakuwaambia sisi ametuambia msikubali kucheza nao tena. 

Huku nyumbani kwa watoto wa simba wakaambiwa wamechezea bahati wangepata kitoweo cha kutosha basi palipokucha watoto hao wakawa wa kwanza kufika bondeni wakawaita watoto wa swala walipowasikia wakawaambia “Kama mama yenu hakuwaambia sisi ametuambia” .

Kwa miaka mingi watanzania wamekuwa wakarimu na wamekuwa wakiwapokea wageni hata bila ya kuwajua,kuwafikisha kwa balozi wa nyumba kumi ,hali hii imekua ikiwagharimu kwani wageni kutoka nje ya nchi wako ambao ni wabaya na wana nia ovu matokeo yake yanaweza kuwa haya ya mfululizo wa matukio ya milipuko ya mabomu.

Nchi ya Tanzania ni nchi pekee ambayo mgeni anaweza kuishi bila hofu wala wasiwasi huku akitamba hata kama hana uhalali wa kuwepo nchini na hata kama shughuli anazozifanya  hazieleweki na zinatiliwa shaka na watu,Watanzania wengi hawajali wanachulia kawaida na hivyo kutoa mwanya kwa watu hao kuidhuru nchi yetu. 

Hii ni hatari tunayoitengeneza wenyewe kwa kuendekeza ukarimu  unaotugharimu kutuangamiza baadae mfano hili la mabomu.

Mfano mzuri ni nchi ya Kenya waliwakaribisha raia wa Somalia na kuishi nao kama ndugu wakazaliwa huko na hata kufia huko linapokuja suala la kupigana na wapiganaji wa  Alishaabab inawawia vigumu kujua msomali yupi ni salama na yupi anahusika kwasababu ni vigumu kuwatambua tatizo hilo linawaangamiza.

Ni ukweli kuwa Tanzania imezungukwa na nchi 8 na ina mipaka 9 ,mpaka mkubwa kuliko yote ni bahari na unaingiza watu wema na wabaya. 

Tutawatambuaje hawa wabaya wanaotumia vibaya ukarimu wetu kama daraja la kupitisha na kutekeleza uovu walioupanga dhidi ya nchi yetu.

Hatusemi tusiwe wakarimu bali tuzidishe umakini na sio woga wala wasi wasi ili ukarimu wetu usitumiwe vibaya na watu wenye nia mbaya.

Tabia ya kupuuzia mambo madogo nayo inatugharimu kwani hayo madogo ndiyo yanazaa makubwa na ukiona jambo kubwa ujue lilianza na jambo dogo.

Hata maandiko matakatifu yanaeleza wazi kuwa “Ukipuuzia  mambo madogo madogo utaanguka kidogo kidogo”.

Na haya maanguko madogo madogo ni mabaya sana ni kama kansa inayotula taratatibu bila kujua mwisho wa siku tukija kushtuka tumeliwa tumeisha.

Tusisubiri kunaguka na kuisha tuwe wakarimu lakini tusizidi san asana tuzidishe umakini hasa katika kipindi hiki ambacho tunaona milipuko ya mabomu imekithiri hasa katika mkoa wa Arusha,kwasababu wakizidisha ukarimu utachukuliwa kama udahaifu kwa maadui wakati si tunaona ni kitu cha kujivunia .Mwimbaji mmoja wa rege alitunga wimbo unaoitwa “My kindness for weakness”.

Ni  kweli kabisa ukarimu wetu umekua ukichukuliwa kama udhaifu wetu ,watu wabaya wanautumia vibaya kama mwanya wa kupitisha mambo yao mabaya.

Suala la Watanzania  kusajiliwana  na kupatiwa vitambulisho vya taifa litasaidia Watanzania kutambuana na kutambulika rasmi kama raia na mabenki,taasisi za fedha,uhamiaji na mamlaka nyingine na katika huduma za jamii.

Vitambulisho vya taifa vinavyotolewa na Mamlaka husika ya Taifa yaani NIDA,wanasaidia kutengeneza taarifa za raia kitaifa (national data base) ambayo itatumika katika masuala ya ulinzi na usalama wa nchi na pia kulisaidia jeshi la polisi linalopambana na uhalifu wa ndani na unaotoka nje ,polisi  watafanya kazi yao kwa ufanisi zaidi.

Tunalo jukumu la kulinda nchi yetu tusitegemee watu kutoka nje ya nchi ndio watakuja kutulindia nchi yetu,amani ni msingi wa kila kitu bila amani hakuna shughuli zozote za kimaendeleo zinazoweza  kufanyika iwe kilimo,elimu.

Tanzania isije ikageuka chaka la uovu tumeona mkoa wa Arusha unavyozidi kutikiswa na matukio ya milipuko ya mabomu .

Wananchi waamke watoe taarifa juu ya watu wanaoingia nchini kinyamela na kutekeleza nia zao mbaya ni hatari sana kwa taifa kuendelea kulea uozo na uovu kwa kigezo cha ukarimu.

Ni bora ukarimu wenye umakini ndani yake kuliko ujasiri wenye uharibifu ndani yake.

TUCHUKE TAHADHARI KABLA YA HATARI

Mawasiliano: ferdinandshayo@yahoo.com

 

error: Content is protected !!