Friday , 3 February 2023
Habari Mchanganyiko

Ukame janga jipya Afrika

Hali ya ukame katika moja ya maeneo ya Afrika kwa sasa
Spread the love

 

KUONGEZEKA kwa shughuli za kibinadamu zisizo rafiki kwa mfumo wa ikolojia katika Bara la Afrika na nchi nyingine zinazoendelea duniani, kumetajwa kuwa sababu za uharibifu wa ardhi na ukame. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamebainishwa katika mkutano wa jukwaa linaloshughulika na masuala ya uhifadhi wa mazingira (Global Landscape Forum), uliofanyika kwa njia ya mtandao kwa muda wa siku mbili, tarehe 2 hadi 3 Juni 2021.

Akizungumza katika mkutano huo, Rais wa Taasisi ya Muungano wa Mapinduzi ya Kijani barani Afrika (AGRA), Agnes Kalibata, alisema chanzo kikubwa cha uharibifu wa ardhi na ukame, ni shughuli za kilimo na ukataji miti.

Kalibata alitaja sababu nyingine kuwa ni, ufugaji wa kuhama hama na matumizi ya mkaa na kuni yaliyokithiri, yanayosababisha kuongezeka kwa vitendo vya ukataji miti holela.

Rais wa AGRA, Agnes Kalibata

“Shughuli zote hizi za kibinadamu si rafiki kwa mazingira na mifumo ya ikolojia , ambapo huchangia kwa asilimia 80 mabadiliko ya tabia ya nchi, kupotea kwa mimea anuwai na kuleta utapiamlo kutokana na kushuka kwa uzalishaji mazao ya chakula, katika maeneo yenye ukame,” alisema Kalibata.

Rais huyo wa AGRA, alisema tatizo la utapiamlo kwenye maeneo yenye ukame haliwezi kuisha kwani watu wake wanakosa madini muhimu yatokanayo na mimea, kama zinki, kalsiamu na chuma.

Kufuatia changamoto hizo, Katibu Mkuu Kiongozi wa Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP), Inger Anderson, alitoa wito kwa nchi zinazoendelea kuchukua juhudu za haraka na za makusudi, kuhamasisha uhifadhi wa mazingira.

Anderson alitoa wito kwa nchi zilizoendelea na jumuiya za kimataifa, kupitia utekelezwaji wa Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGS), kuziwezesha nchi zinazoendelea kukabiliana na ukame, ikiwemo kuzipatia fedha na utaalamu wa kuondoa ukame.

Katibu Mkuu Kiongozi wa UNEP, Inger Anderson

“Ni fursa nzuri kuanza kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, ili tuweze kuunda ulimwengu wenye ustawi, mafanikio na usawa,” alisema Anderson.

Mtendaji huyo wa UNEP alisema, ukame unaonedleea kuishamiri barani Afrika, ni tishio kwa dunia nzima, kwa kuwa bara hilo linatoa asilimia 44 ya mazao ya chakula na mifugo, yanayotumika duniani kote.

Pia, Anderson alisema, Afrika inachukua asilimia 40 ya watu, ambao ni nguvu kazi ya ulimwengu.

“Tunahitaji kupata fedha kwa ajili ya kusaidia nchi zenye ukame, lakini pia kujikita kwenye uwekezaji unalolinda mazingira ,” alisema Anderson.

Naye, Katibu Mtendaji wa Mkutano wa Umoja wa Kimataifa wa Kupambaana Ukame (UDCCD), Ibrahim Thiaw, alitoa wito kwa jamii kumaliza tatizo la ukame Afrika, kwa kugeuza changamoto hiyo kuwa fursa , hasa kwa kuwashirikisha vijana.

Katibu Mtendaji wa UDCCD, Ibrahim Thiaw

Makamu wa Rais wa Taasisi ya Rasilimali za Dunia, Wanjira Mathia, alitoa wito kwa jumuiya za kimataifa, kuwaunga mkono vijana waliojitosa kupambana na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Kwa kuunda sera zitakazowezesha kutekeleza maukumu yao kwa ufanisi pamoja na kuwawezesha kiuchumi.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo cha Eldoret nchini Kenya, Prof. Wilson Ng’etech, sekta binafsi zinapaswa kuwajibika katika shughuli za uhifadhi wa mazingira.

Mkutano huo uliwashirikisha watalaamu mbalimbali wa mazingira duniani na waandishi wa habari, umefanyika kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira duniani , inayoazimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka.

Siku hii ilipitishwa na Umoja wa Mataifa (UN), ili kutoa nafasi kwa jamii kujadili masuala mbalimbali yanayohusu mazingira na changamoto zake, ili kutafuta majibu ya changamoto hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

Habari Mchanganyiko

Ndege ya Precision Air yaahirisha safari kwa hitilafu, nyingine yatua kwa dharura

Spread the love  NDEGE ya Shirika la Precision Air imeshindwa kufanya safari...

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa tiba hospitali Mtwara  

Spread the loveBENKI ya NMB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa vifaa...

error: Content is protected !!