Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Ukaguzi wa magari: TBS yaingia kigugumizi
Habari MchanganyikoTangulizi

Ukaguzi wa magari: TBS yaingia kigugumizi

Sehemu ya magari yakiwa bandarini yakisubiri kutolewa na wamiliki wake
Spread the love

 

SHIRIKA la Viwangoa Tanzania (TBS), limeshindwa kueleza iwapo gari litashindwa kukaguliwa ndani ya siku saba, tozo ya kuhifadhi gari hilo bandarini zitatolewa na nani. Anaripoti Brightness Boaz, Dar es Salaam …. (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo Ijumaa tarehe 22 Januari 2021, Roida Andusamile, mesemaji wa TBS amesema, iwapo changamoto hiyo itajitokeza, watajua cha kufanya.

“Sisi tulivyojipanga ni kwamba, tutafanya ndani ya muda uliopangwa. Sasa ikitokea matatizo, ndio hapo tutajua la kufanya lakini kwa sasa hivi tulivyojipanga, tunajua hatutachelewesha,” amesema.

MwanaHALISI Online lilimuuliza swali hilo baada ya mfanyabiashara Leonard Josephat, Mkurugenzi wa Kampuni ya B-Mcars Dealers, kueleza wasiwasi wake juu ya gharama hizo.

“Meli moja ina uwezo wa kushusha magari 1,000 hadi 2,000, je? bandari itaweza kuhudumia na kufanya ukaguzi wa magari yote yatakayoingia nchini kwa mara moja?” amehoji na kuongeza:

“Kitu kingine, je wanavyo vifaa vya kutosha kuhakikisha ukaguzi huo unafanyika ndani ya siku saba pale bandarini? tuna muda wa siku saba wa kutunza mizigo pindi unapofika bandarini, ukizidi unaanza kulipia, nani ataingia gharama hizo?”

Roida amesema, shirika hilo limejipanga kuhakikisha linafanya kazi ndani ya muda huo na wamejipanga vilivyo kwani wana vifaa vya kutosha.

“Tutakagua ndani ya muda huo (wa siku saba), ndio maana tumejipanga, tuna uwezo na tutashirikiana na taasisi nyingine kuhakikisha kuna kuwa hakuna urasimu wowote,” amesema Roida

Akizungumzia vitendea kazi amesema, TBS ina vifaa vya kutosha kuhakikisha kazi hiyo inafanywa kwa wakati.

Tarehe 20 Januari 2021, TBS ilitoa taarifa kwa umma kuwa, magari yote yaingiayo nchini, yatakaguliwa kabla ya kuingizwa mtaani ambapo utaratibu huo utaanza rasmi 1 Machi 2021.

“Utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi utafanyika baada ya kuwasili hapa nchini. Hivyo, magari yote yatakayosafirishwa kuanzia tarehe 1 Machi 2021, yatakaguliwa katika bandari ya Dar es Salaam,” ilieleza taarifa hiyo ya TBS iliyosainiwa na Roida.

Roida alisema, magari yote yatakayopimwa bandarini na kutokidhi matakwa ya kiwango yatahitaji kufanyiwa matengenezo nje ya bandarini na kisha kupelekwa tena kupimwa kwenye yadi ya UDA mkabala na Bandari ya Dar es Salaam.

“Shirika litaendelea kuhakikisha magari yote yaliyotumika na kuingizwa nchini, yanakidhi matakwa ya kiwango cha magari yaliyotumika,” alisema Roida.

Kabla nya mabadiliko ya utaratibu huo, TBS ilikuwa ikifanya ukaguzi nje ya Tanzania kupitia mawakala watatu kutoka Japan na mmoja kutoka Dubai ambao mikataba yao itakoma hivi karibuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mchina wa SGR aburuzwa kortini kwa kumjeruhi Mtanzania, TRC waja juu

Spread the love  RAIA wa China, Zheng Yuan Feng, amefikishwa mahakamani kwa...

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

error: Content is protected !!