November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ujumbe wa mwisho wa Bilionea Mufuruki kwa familia yake

Marehemu Ali Mufuruki

Spread the love

ADIL Mufuruki, mdogo wa marehemu Ali Mufuruki, ameeleza ujumbe wa mwisho ulioachwa na mfanyabiashara huyo maarufu barani Afrika, kwa familia yake. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Adil ameeleza kuwa, marehemu Mufuruki kabla ya umauti kumfika, aliihimiza familia yake kushikama ili iweze kusimama imara.

Adil ameeleza hayo wakati akizungumza kwa niaba ya familia ya Mufuruki, katika shughuli ya kuuaga mwili wa bilionea huyo, iliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Amesema kifo cha Mufuruki kimeacha  pigo kwa familia yake, lakini jambo la Kumshukuru Mungu ni kwamba, kaka yao alitoa muongozo kwa ndugu zake, juu ya namna ya kusimama imara.

“Sisi familia tumepata pigo, lakini tunamshukuru Mwenyezi Mungu kaka yaetu alitupa muongozo, na hatujui labda alijiua, kwa sababu alikuwa anatuandaa kwamba jitahidini kusimama,” ameeleza Adil.

Wakati huo huo, Adil amesema watajifunza mengi kutoka kwa Mufuruki, ikiwemo misimamo yake pamoja na uvumilivu.

“Ali tulimtegemea katika familia kwa fikra na mawazo yake, na sisi kama wadogo zake tukiwa tumekinzana tunajua kuna kaka yetu, alikuwa mtu imara kama wazazi wetu waivyokuwa imara. Alikua anatuunganisha tunakuwa pamoja,” amesema Adil na kuongeza;

“Tulichojifunza kwake ni uvumilivu, kwa hiyo tumejifunza mengi kwake, tunamshukuru mungu kwamba katuonesha njia.”

Mwili wa Mufuruki unatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mufuruki alifariki dunia Jumamosi ya tarehe 7 Desemba 2019.

error: Content is protected !!