May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ujumbe wa mwanaye Manumba waliza wengi

Spread the love

 

SAA chache baada ya Mkurugenzi Mstaafu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba, kufariki dunia, mwanaye Rose ameandika ujumbe wa kusisimua kumuaga baba yake kiasi cha kuwaibua viongozi mbalimbali na kumpa pole. Anaripoti mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kupitia kwenye akaunti yake ya Instagram, Rose Manumba ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Kigoma, ameandika hivi; Baba Yangu Robert Manumba, Ahsante kwa kunionyesha maana halisi ya upendo wa baba kwa mtoto.

“Ahsante kwa kuamini katika juhudi zangu kuwa naweza kuwa bora katika chochote kile nachotaka kuwa.

kwenye furaha tulicheka pamoja na kwenye huzuni tulilia Pamoja lakini leo (tarehe 30, 2021) umetangulia mbele za haki na kuniacha.

“Sikuzote za maisha yangu nimejivunia kuwa na baba kama wewe na nashukuru umeishi ukilijua hilo na sitoacha kujivunia katika maisha yangu mpaka tutapokutana tena. nitakupenda milele.

“Mwenyezi Mungu akupumzishe kwa amani baba yangu mpenzi Robert Manumba.”

Kufuatia ujumbe huo, Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo na viongozi wengine wamejitokeza na kumpa pole Rose.

Joanfaith Kataraia naye aliandika hivi “Pole sana mpendwa, Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu”.

Mkuu wa wilaya ya Songwe, Simon_simalenga’ ameandika pole sana mdogo wangu @rosemanumba. Mzee Robert Manumba alikuwa ni mtu mwema sana sana. Pole sana ndugu yangu

Wakati Katibu Mkuu wa UVCCM,  Kenani Kihongosi aliandika “tunakuombea pia tunamuombea mzee wetu Mungu akupe nguvu na uvumilivu @rosemanumba”.

error: Content is protected !!