Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Ujumbe wa mwanawe Museveni kwa Uhuru waibua mjadala
Kimataifa

Ujumbe wa mwanawe Museveni kwa Uhuru waibua mjadala

Spread the love

 

Mwanawe Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba amemwandikia Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ujumbe ulioibua mjadala mzito miongoni mwa mataifa hayo mawili hasa ikizingatiwa kumekuwapo na mvutano kuhusu utaratibu wa vipimo vya Corona katika mpaka wa Malaba. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Aidha, katika kile kilichoonekana kujibu hoja zinazoibuliwa kuhusu mzozo huo, Kainerugaba kupitia mtandao wa kijamii siku ya Jumapili tarehe 16 Januari 16, alisema hakuna kitakachoweza kuvunja uhusiano kati ya Kenya na Uganda.

Japo hakufafanua zaidi ujumbe wake, ujumbe huo ulizua mjadala mkali kwani ameutoa wakati mvutano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili ya kanda ya Afrika Mashariki ukizidi kufukuta.

“Yeyote anayefikiri anaweza kuvunja uhusiano kati ya Uganda na Kenya aende kwanza kumwomba Yesu Kristo msamaha! Mungu ibariki Uganda na Kenya,” aliandika.

MZOZO WA KIBIASHARA

Uganda inakabiliwa na uhaba wa mafuta baada ya madereva Wakenya wanaosafirisha bidhaa hiyo kukataa kulipa Shilingi za Kitanzania 61,000 (KSh3,000) wafanyiwe vipimo vya corona hata kama wana vyeti vinavyoonyesha hawana virusi hivyo. Agizo hilo lilitolewa na Rais Museveni.

Kutokana na madereva hao kugoma, kulikuwa na msongamano mkubwa wa magari ya kusafirisha mafuta kwenye mipaka ya Busia na Malaba.

Aidha, mwishoni mwa wiki iliyopita wizarta ya Kazi nchini Uganda ilitoa taarifa kwa umma na kuahidi kutatua suala hilo ili kuruhusu malori yanayosafirisha mafuta kutozuiliwa.

Serikali ya Uganda katika jitihada za kutatua mgogoro huo, iliorodhesha vituo zaidi vya afya na maabara za kupima corona kwa urahisi.

Hata hivyo, bei ya mafuta imekuwa ikipanda kwa kasi kutokana na mzozo huo lakini serikali ya Uganda imekanusha madai hayo.

“Walanguzi wanaohifadhi bidhaa za petroli na kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta bila utaratibu wameonywa. Bei ya petroli nchini haipaswi kuzidi UShs5,000 (Tsh 104) kwa lita,” ilisoma sehemu ya taarifa kutoka Uganda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

Kimataifa

Mashabiki wakabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya wafuasi wa Arsenal na Manchester City kupigana Uganda

Spread the love  MASHABIKI wawili wa soka nchini Uganda wanakabiliwa na mashtaka...

Kimataifa

China inatathmini upya sera za wafanyakazi

Spread the love  WAKATI idadi ya watu wa nchi China inapungua, Beijing...

error: Content is protected !!