September 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ujumbe wa Dk. Ndugulile kwa Rais Samia

Dk. Faustin Ndungulile

Spread the love

 

DAKTARI Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni (CCM) amemahukuru Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kumpa nafasi ya kuhudumu kwenye serikali yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Ndugulile ametoa shukuran hizo leo Jumatatu, tarehe 13 Septemba 2021, saa chache kupita tangu, Rais Samia kumuapisha Dk. Ashatu Kijaji kushika nafasi yake kwenye wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari.

Ni baada ya Rais Samia kufanya mabadiliko madogo kwenye baraza lake la mawziri kwa kuteua wapya akiwemo Dk. Kijaji ambaye pia ni Mbunge wa Kondoa.

Wizara hiyo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) ni mpya ambayo ilianzishwa Desemba 2020 wakati wa utawala wa Hayati Rais John Magufuli na waziri wa kwanza kuiongozo alikuwa Dk. Ndugulile.

Hata hivyo, Rais Samia ameifanyia mabadiliko kwa kuchukua Idara ya Habari kutoka wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kuipeleka wizara ya tehama na sasa inajulikana kama wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari na Waziri wake ni Dk. Kijaji.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Dk. Ndugulile ameandika “Namshukuru sana Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika Serikali yake.”

“Nawashukuru Wizara na Taasisi zake kwa ushirikiano walionipa. Nashukuru wadau wa TEHAMA kwa ushirikiano mlionipa. Hongera sana Mhe Dkt Ashatu Kijaji kwa kuteuliwa. Kazi Iendelee,” amesema

error: Content is protected !!