December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ujumbe wa Dk. Mashinji baada ya kutoka jela

Dk. Vincent Mashinji

Spread the love

DAKTARI Vincent Mashinji, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mwanachama mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametuma salamu za pongezi kwa wanachama wa chama chake cha sasa. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).  

Amesema, amefurahishwa na hatua ya wanachama wa chama hicho kwa umoja na mapenzi, kujikusanya na kumchangia kiasi cha Sh. 30 milioni zilizomuwezesha kutolewa jela.

Mwanachama huyo wa CCM ametoa kauli hiyo leo tarehe 11 Machi 2020, muda mfupi baada ya kutoka jela.

Dk. Mashinji amelipiwa faini ya Sh. 30 mlioni na CCM, baada ya jana kuhukumiwa kwenda jela miezi mitano ama kulipa faini kwenye kesi ya uchochezi Na. 112/2018.

Dk. Mashinji alikumbwa na kesi hiyo alipokuwa Katibu Mkuu wa Chadema, baadaye alihamia CCM.

Dk. Mashinji na wenzake wa Chadema, walihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwenda jela miezi mitano ama kulipa jumpa ya Sh. 350 milioni, baada ya kukutwa na makosa 12 kati ya 13 waliyotuhumiwa.

Baada ya hukumu hiyo iliyosomwa na Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakam hiyo, wote tisa walipelekwa katika gereza la Segerea.

Leo kuanzia asubuhi, Humprey Polepole ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, aliendesha zoezi la kwenda huku na kule katika hatua za kukamilisha utaratibu na vibali vya kumtoa Dk. Mashindi vinapatikana.

Hata hivyo, Freeman Mbowe na viongozi wenzake wa Chadema, wamebaki jela wakati mfungwa mwenzao, Dk. Mashinji akitoka.

error: Content is protected !!