May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ujumbe wa Amnest kwa Rais Samia huu hapa

Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spread the love

 

SHIRIKA la Kimataifa la Kutetea Haki za Binaadamu (Amnesty International), limeshauri Serikali ya Tanzania kutumia kamati ya corona iliyoteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushughulikia upatikanaji chanjo. Vyombo vya kimataifa vinaripoti … (endelea).

Katika taarifa hiyo iliyochapwa kwenye mtandano wa shirika hilo, Amnest imesifu hatua ya Rais Samia kutangaza tume ya kushughulikia virusi vya corona (COVID-19), na kwamba matumaini ya kupambana na corona yanaonekana.

Shirika hilo limeripoti kwamba, bado kuna kazi kubwa ya kukabiliana na virusi hivyo Tanzania, na kwamba ni wakati kwa tume hiyo kufanya utaratibu wa kupata chanzo kama ilivyo kwa mataifa mengine.

Taarifa hiyo imeeleza, Tanzania chini ya uongozi wa Hayati John Magufuli, kulikuwa na ukimya wa muda mrefu kuhusu mapambano dhidi ya virusi hivyo.

Amnesty limeeleza, iwapo chanjo hiyo itapatikana, Serikali ya Tanzania inapaswa kuhakikisha inaisambaza katika maeneo mbalimbali ya nchi, na kusiwe na ubaguzi.

error: Content is protected !!