Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ujio wa Lissu ‘bab kubwa’
Habari za SiasaTangulizi

Ujio wa Lissu ‘bab kubwa’

Spread the love

UJIO wa Tundu Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, utakuwa wa kipekee. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Lissu ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg, nchini Ubelgiji, amesema hatokuja peke yake. Atasindikizwa na wanadiplomasia wa kimataifa.

“Zaidi ya hayo, vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa, pamoja na marafiki wa Tanzania katika jumuiya ya kimataifa wangependa kujua siku na tarehe ya kurudi kwangu, ili waweze kufuatilia tukio hili muhimu kwa ukaribu zaidi.

“Katika hali ya kipekee, kuna wawakilishi wa taasisi za kidini na kijamii, ndani na nje ya nchi yetu; wanadiplomasia kutoka nchi rafiki na mashirika ya kimataifa, pamoja na wawakilishi wa vyombo vya habari vya kimataifa, ambao wameonyesha nia ya kunisindikiza katika safari yangu ya kurudi nyumbani,” ameandika Lissu kwenye waraka wake aliousambaza katika mitandao ya kijamii tarehe 7 Septemba 2019 kuhusu kurejea kwake.

Katika ujio wake huo, Lissu amesema,  anazungumza na wawakilishi wa nchi marafiki wa Tanzania, mashirika na taasisi za kimataifa na za kikanda na mashirika ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kuhakikisha usalama wake.

Ikiwa miaka miwili tayari imepita baada ya kushambuliwa kwa risasi 36, ‘Area D’ jijini Dodoma, tarehe 7 Septemba 2017, Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema sasa anasubiri ruhusa ya madaktari wake ili arejee nchini.

Kwenye waraka wake, Lissu ameeleza kuwa hana hofu ya kurejea nchini, “mimi sio mhalifu, kwa hiyo siwezi kurudi nyumbani kwetu kwa kificho.”

Ameandika “Naomba niweke jambo moja wazi. Hili ni kuhusu uwazi wa tarehe ya kurudi kwangu nyumbani. Baadhi ya watu, kwa kuelewa kuwa watu waliotumwa kuja kuniua bado wanaitwa ‘watu wasiojulikana’, wamenishauri kwamba tarehe ya kurudi nyumbani iwekwe siri mpaka siku yenyewe ya safari ya kurudi nyumbani.

“Watu hawa wenye nia njema wanaamini kwamba, siku ya kurudi nyumbani ikiwa siri, basi ‘watu wasiojulikana’ na wale wanaowatuma hawatafahamu kuhusu ujio wangu, na kwa hiyo nitakuwa salama.”

Lissu ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amesema, “pamoja na nia njema yake, siafikiani na ushauri huu.”

Amesema, atarudi nyumbani mchana kweupe mbele ya macho ya Watanzania na ya dunia nzima, na kwamba safari yake itafanyika baada ya mashauriano kuhusu siku na utaratibu mzuri na salama zaidi wa kurudi kwake nyumbani.

“Siku na utaratibu tutakaokubaliana, utatoa muda wa kutosha kufanya maandalizi yote yanayohitajika, ndani na nje ya Tanzania. Siku na utaratibu huo utatangazwa kwa umma katika muda muafaka,” amesema Lissu na kuongeza;

“Nimezungumza pia na ninaendelea kuzungumza na viongozi mbalimbali wa kisiasa, kidini na wa taasisi za kijamii nchini kwetu.”

Lissu amesema, Watanzania wengi ambao wamemwombea au kunichangia fedha na rasilmali zilizomwezesha kuishi na kupatiwa matibabu Kenya na Ubelgiji, wangependa kuja kwa wingi kumpokea uwanja wa ndege siku hiyo.

“Mimi mwenyewe ningependa kupokelewa na watu wengi iwezekanavyo, baada ya yote ambayo nimepitia, na ambayo nchi yetu imepitia, tangu Septemba 7, 2017.

“Zaidi ya hayo, vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa, pamoja na marafiki wa Tanzania katika jumuiya ya kimataifa wangependa kujua siku na tarehe ya kurudi kwangu, ili waweze kufuatilia tukio hili muhimu kwa ukaribu zaidi,” amesema na kusisitiza kwamba siku ikifika ataeleza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!