Monday , 30 January 2023
Home Kitengo Maisha Burudika Ujio wa Asa na ngoma mpya ‘Ocean’
Burudika

Ujio wa Asa na ngoma mpya ‘Ocean’

Spread the love

MWANAMUZIKI mahiri kutoka nchini Nigeria, Bukola Elemide maarufu kama ‘Asa’ ameachia ngoma yake mpya iitwayo Ocean aliyofanya na prodyuza maarufu, Prime, ikiwa ni maandalizi ya kutoa albamu yake ya V (Five) inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni. Anripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Kuachiwa kwa ngoma hiyo, kunakuja muda mfupi baada ya mwanadada huyo, kutoa ngoma nyingine, Mayana ambayo imepokelewa vyema na mashabiki wa muziki ndani na nje ya mipaka ya Nigeria.

 

Dairekta mkali, Meji Alabi ndiye aliyefanya video ya wimbo huo ambapo kwa kuzingatia mashairi na staili ya uimbaji ya Asa, ukichanganya na vionjo alivyoviweka dairekta huyo katika video hiyo iliyopo katika mfumo wa ‘visuals’, kwa pamoja vimeifanya video hiyo kuwa moto wa kuotea mbali.

Akiuzungumzia wimbo huo, Asa amenukuliwa akisema: “Ocean ni miongoni mwa kazi bora kabisa katika tasnia ya muziki. Nguvu za kujua mimi ni nani, nini nakitaka, kufanya ninachokitaka na kuishi maisha ya ukamilifu kama Mungu alivyoniumba.”

Ocean ni miongoni mwa ngoma zilizopo kwenye albamu ya V (Five) ya mwanadada huyo inayotarajiwa kuingia mitaani Februari 25 na ilitengenezwa dakika za mwisho kabla mwanadada huyo hajaamua kurudi Nigeria baada ya ziara za kimataifa za muziki, kuahirishwa kutokana na janga la Corona.

Pia mwanadada huyo anatarajia kufanya shoo jijini London, Uingereza Mei 3, 2022 katika Ukumbi wa Royal Albert Hall, ikiwa ni mwendelezo wa kuutangaza muziki wake kimataifa. Cheki video ya wimbo huo hapa: https://youtu.be/MIKNaODK4jk

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Burudika

NMB yawakutanisha Jay Meleody, Navy Kenzo Z’bar

Spread the loveMSANII wa kizazi kipya, Jay meleody akitumbuiza kwenye tamasha la...

Burudika

Man Mo; Mkali aliyetajwa na Hayati Magufuli mkutanoni

Spread the loveKILA mtu ana kipaji chake alichozaliwa nacho hapa duniani. Shida...

Burudika

Netta, Mr Eazi waangusha kolabo kali ‘Playground Politica’

Spread the loveMSANII maarufu wa muziki wa Pop, Netta amemshirikisha staa mkubwa...

Burudika

Kibao kipya cha Mr Eazi; Personal Baby

Spread the loveSTAA wa muziki kutoka nchini Nigeria, Mr Eazi ameachia ngoma...

error: Content is protected !!