Saturday , 15 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Ujerumani yaipa Tanzania msaada wa Bil 330
Habari Mchanganyiko

Ujerumani yaipa Tanzania msaada wa Bil 330

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imepewa msaada wa zaidi ya Sh. 330 bilioni na Serikali ya Ujerumani. Ni kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji safi na salama na kilimo cha umwagiliaji. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Msaada huo ni kupitia Benki yake ya Maendeleo (KfW) pamoja na Mfuko wa Kimataifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi (Green Climate Fund).

Makubaliano ya mikataba hiyo baina ya Serikali na Ujerumani yamefanyika tarehe 3 Aprili 2019, na kusainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW), anayeshughulikia Ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya, Dk. Klaus Mueller.

Akizungumza baada ya makubaliano hayo, Dotto amesema, katika mkataba wa kwanza, kiasi cha Sh. 265 bilioni kimetoelwa na Mfuko wa Kimataifa wa Kuakabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi (Green Climate Fund) na mkataba wa pili unahusisha Sh. 65 bilioni ambazo zimetolewa na KfW.

Amesema, fedha hizo zitatumika Mradi wa Maji wa Simiyu utajengwa kupitia Ziwa Victoria, pamoja na miradi ya kilimo endelevu cha umwagiliaji, usafi wa mazingira, maji na malisho ya mifugo na miradi ya kuzijengea uwezo taasisi zitakazotekeleza miradi hiyo hasa mamlaka za maji katika wilaya tano za Bariadi, Itilima, Meatu, Busega na Maswa.

Dotto amesema, katika kipindi cha miaka mitatu, Serikali ya Ujerumani imeipatia Tanzania zaidi ya Sh. 518.5 bilioni kwa ajili ya utekjelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za afya, nishati, uhifadhi wa maliasili, udhibiti wa fedha za umma na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Naye,   Dk. Mueller amesema mradi wa maji wa Ziwa Victoria katika mkoa wa Simiyu, utanufaisha watu zaidi ya 500,000 pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuhifadhi vyanzo vya maji, usafi wa mazingira na kuendelesha kilimo bora chenye kuhifadhi mazingira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DAWASA yaja na suluhisho la maji kwa wakazi wa Sinza C,D

Spread the loveWakazi wa Kata ya Sinza, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Samia: Wakuu wa mikoa, wilaya wanaendeleza ubabe

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema bado wakuu wa wilaya na...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Vitalu 19 vya madini vyazalisha ajira 12,000 Songwe

Spread the loveZAIDI ya vijana 12,000 kutoka Wilaya ya Songwe mkoani Songwe...

Habari Mchanganyiko

Mmoja auawa kwa tuhuma za kuiba sokoni, Polisi walaani

Spread the loveMwanaume mmoja ambaye hajafahamika jina lake  ameuawa  na wananchi wenye...

error: Content is protected !!