May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ujerumani kuunda serikali ya mseto

Spread the love

 

WAJERUMANI wameamua. Ndivyo unavyoweza kutafsiri matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 26 Septemba mwaka huu nchini humo, baada ya kuupiga chini muungano wa kihafidhina wa CDU na CSU ambao umekuwa ukiongozwa na Kansela Angela Merkel anayemaliza muda wake. Anaripoti Victoria Mwakisimba –TUDARCo.

Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yanaonesha kuwa chama cha SPD kimepata ushindi mwembamba wa asilimia 25.7 na kukishinda chama cha Kansela Merkel cha CDU ambacho kimeibuka katika nafasi ya pili kwa asilimia 24.1

Kutokana na matokeo hayo Kiongozi Mkuu wa chama hicho cha SPD, Olaf Scholz amesema anatarajia kuunda haraka serikali ya mseto kabla ya kufikia mwezi Disemba mwaka huu.

Ametoa wito wa kuharakishwa makubaliano ya kuundwa serikali ya mseto kwa kuwa uchaguzi huo umeshindwa kutoa mshindi wa moja kwa moja.

Wito wa Sholz umekuja saa chache baada ya matumaini ya kuunda serikali hiyo kuanza kufifishwa na mgombea wa ukansela kupitia muungano wa CDU/CSU, Armin Laschet ambaye anataka kurefusha mchakato wa kutafuta serikali mpya nchini humo.

Iwapo muungano wa Kansela Merkel ambao umedumua madarakani kwa miaka 16 hautaridhia kuchukua nafasi ya upinzani, utalazimika kuchuana na SPD kuvishawishi vyama vingine ikiwemo kile cha walinzi wa mazingira na waliberali wa FDP kuunda serikali ijayo ya mseto.

error: Content is protected !!