Friday , 1 March 2024
Home Kitengo Biashara Ujenzi waiva barabara ya Bigwa – Kisaki
Biashara

Ujenzi waiva barabara ya Bigwa – Kisaki

Innocent Bashungwa, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo
Spread the love

WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa mkandarasi atakayetekeleza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Bigwa – Mvuha – Kisaki (km 133.28), sehemu ya Bigwa – Mvuha (km 78) ameshapatikana.

Ameongeza kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba wa ujenzi wa sehemu hiyo ya barabara. Anaripoti Danson Kaijage, Morogoro (endelea)

Bashungwa ameeleza hayo wakati akizungumza na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale, wakati alipoombwa kutoa ufafanuzi kwa wananchi wa kata ya Mkuyuni wilayani Morogoro Vijijini kuhusu ujenzi wa barabara hiyo.

“Barabara hii itajengwa na mkandarasi China Railway 15 bureau group corporation na upembuzi yakinifu sambamba na usanifu wa kina kwa km 78 kuanzia Bigwa umeshakamilika,

“Sasa hivi tupo kwenye hatua za mwisho za kusaini mkataba wa kuanza kujenga kwa Kiwango cha lami,” amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa ameeleza baada ya taratibu za kusaini mkataba kukamilika, ataambatana na Mbunge huyo kufika jimboni hapo kumtambulisha mkandarasi na kumkabidhi kwa wananchi kwa aijli ya kuanza utekelezaji.

Naye, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha za kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Biashara

Meridianbet yaimarisha usafi Kijitonyama

Spread the loveMABINGWA wa michezo ya kubashiri kampuni ya Meridianbet leo imefanikiwa kufika...

Biashara

Kampeni SBL ya unywaji pombe chini ya umri yafika Kilimanjaro

Spread the loveKAMPUNI ya bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL) inewahimiza wanafunzi...

Biashara

Cheza Pragmatic Play na ushinde mgao wa Bil 12 za Meridianbet kasino

Spread the love  HII habari njema kwa wapenzi wote wa michezo ya...

error: Content is protected !!