August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ujenzi wa VETA wagusa maisha ya vibarua Mkinga

Spread the love

WANANCHI wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga wameeleza kufaidika na miradi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ambayo inajenga chuo cha ufundi wilaya hapo chenye madarasa 17 na karakana sita. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yameleezwa hivi karibuni na Meshack George anayefanya kazi kama fundi msaidizi katika mradi huo ambapo pamoja na mambo mengine ameishukuru Serikali kwa kuleta mradi huo ambao umemuwezesha kununua shamba na mabati kwa ajili ya kuanza ujenzi wa nyumba yake binafsi.

Mbali na Meshaki wanufaika wengine wakubwa wa mradi huo unaoendelea wilayani Mkinga, ni wananchi wanaofanya kazi kama vibarua.

Mwanahamisi Jumbe ambaye ni bibi wa miaka 70 anafanya kazi mbalimbali katika kukamilisha mradi naye pia ameeleza kufaidika na mradi huo.Amesema anafanya kazi zozote ikiwemo kuchimba mitaro na kufanya usafi.

“Mradi huu umeninufaisha sana, kwa sababu nikipata hela hapa, nikienda nyumbani ninaenda kujiendeleza. Mimi ni mfanyabiashara ndogondogo maandazi na nyinginezo, nikipata hela naenda kujiendeleza zaidi” amesema Mwanahamisi.

Vibarua hao wananufaika kutokana na maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassana, kwamba miradi inayojengwa nchini kote itoe kipaumbele kwa wakazi wa maeneo husika, ili wawe wanufaika wakuu wa vibarua hivyo.

Aidha, akifafanua kuhusu mradi huo Renatus Kagya ambaye ni Msimamizi wa Mradi amesema Chuo cha VETA kinachojengwa katika wilaya ya Mkinga, kitakuwa na madarasa 17 kwa ajili ya kupokea vijana wa Mkinga na maeneo mengine ya Tanzania.

Amesema lengo la mradi huo ni kuwapa vijana ujuzi utakaowezesha kupambana katika soko la ajira au kijiajiri wenyewe.

error: Content is protected !!