July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ujenzi wa soko wachukua miaka tisa

Soko la Kigogo Fresh B ambalo halijakamilika kwa miaka tisa sasa

Spread the love

NI miaka tisa sasa tangu Halmashauri ya manispaa ya Ilala ianze ujenzi wa soko la Kigogo Fresh, kata ya Pugu. Lakini ujezi wa soko hilo haujamalizika; huku eneo lake lote likiwa limezungukwa na vichaka. Anaripoti Pendo Omary … (endelea).

“Kwa kuwa soko halifanyi kazi. Tunalazimika kununua mahitaji Gongo la Mboto. Tunatumia muda mwingi na gharama kubwa kufika huko,” anasema Mariamu Khamis, mkazi wa mtaa wa Kigogo Fresh B, katika mahoajiano yake na MwanaHALISI Online.

Mbali na usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo, ucheleweshaji wa ufunguzi wa soko hili umeathiri baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo.

Wengi wa wafanyabiashara hawa ni wale waliondolewa pembeni mwa barabara ya kata hiyo, baada ya vibanda vibanda vyao kuvunjwa kwa ahadi ya kupewa vizimba katika soko hilo jipya.

Mariamu anasema, aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa huo, Ally Maguno, alitangazia kukamilisha ujenzi wa vizimba hivyo na kuanza ndani ya siku 17. Hii ilikuwa Octoba mwaka 2013.

Naye Veronika Malima, mkazi wa Mtaa wa Kigogo Fresh B. anasema, kutofunguliwa kwa soko hilo, kumemtia hasara kubwa, kwani “tayari nilikuwa nimekopa Sh. 350,000 kwa ahadi ya kurejesha Sh. 450,000. Hizi fedha nilizutumia kujengea kizimba ndani ya soko.”

Akijibu madai hayo, msemaji wa Manispaa ya Ilala David Langa, amekiri mradi wa soko hilo kuwa bado haujakamilika. Umeme na maji bado havijawekwa na mkandarasi bado anadai fedha zake.

Anasema, mkurugenzi akizilipa hizo fedha, mkandarasi atamalizia ujenzi na kukabidhi soko hilo mara moja. Hakusema lini.

error: Content is protected !!