Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Ujenzi soko la Sabasaba Morogoro wageuka kitendawili
Habari Mchanganyiko

Ujenzi soko la Sabasaba Morogoro wageuka kitendawili

Spread the love

HALMASHAURI  ya Manispaa ya Morogoro imeombwa kuweka wazi na kuanza mapema ujenzi wa soko kuu jipya la kisasa, anaandika Christina Haule.

Soko hilo lilivunjwa miaka minne iliyopita kwa ahadi ya kujengwa lingine la kisasa,lakini mpaka leo hakuna dalili ya ujenzi kuanza.

Mudhihiri Shoo ambaye ni diwani wa kata ya sabasaba alisema hayo jana wakati wa kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Shoo alisema soko hilo lilivunjwa  mwaka 2013 na ujenzi wake ulitarajiwa kuanza  mwishoni mwa mwaka 2013 jambo ambalo mpaka sasa halijafanyika.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga alisema, ujenzi wa soko hilo umechelewa kutokana na kubadilika kwa michoro na kuongezeka kwa gharama za ujenzi na kwamba sasa unatarajia kuanza baada ya fedha kukamilika.

Kubadilika michoro hiyo sasa gharama za ujenzi zimeongezeka kutoka Sh bilioni  10  hadi Sh. bilioni  15  jambo lililofanya benki ya CRDB iliyokuwa na nia ya kuingia mkataba wa kuweka masharti magumu ambayo Manispaa ilishindwa.

Alisema, hali hiyo imesababisha Manispaa kuanza kufanya mazungumzo na benki ya TIB ambayo wamekubaliana kuwakopesha Sh. bilioni 15 kwa ajili ya ujenzi huo.

Aliyataja masharti ambayo wanapaswa kukamilisha kabla ya kupata mkopo kuwa ni pamoja na kuwa na mchoro sahihi wa soko, kuwa na gharama za ujenzi (BOQ), kukamilisha kibali toka Baraza la Usimamizi wa Mazingira Tanzania ( NEMC), kuwa na mpango kazi wa 2016/21, uthamini wa kiwanja na kibali kutoka TAMISEMI.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!