May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ujenzi SGR Mwanza – Isaka kuanza

Spread the love

 

UJENZI wa reli ya kisasa ya (SGR), kutoka Mwanza kwenda Isaka, nchini Tanzania, unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Masanja Kadogosa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), jana Jumanne tarehe 9 Machi 2021.

Kadogosa amesema, kipande hicho (Isala- Mwanza), chenye urefu wa kilomita 341 kitagharimu Sh.3.0267 trilioni.

Amesema, tayari kikao cha pamoja cha wadau wa mradi huo kilifanyika juzi Jumatatu, katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka, Maswa lengo likiwa kuwaweka tayari kuhusu mradi huo.

Masanja Kadogosa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC)

Kadogosa amesema, serikali iliamua kuitisha kikao hicho cha wadau kwa kuwa, mradi huo utahusisha kambi ya watu karibu 3,000 hivyo, ilikuwa lazima kuweka mazingira sawa.

“Hapa Malampaka tutakuwa na kambi ya watu zaidi ya 3000, hivyo ni vizuri wananchi wakaandaliwa ili waweze kushiriki fursa mbalimbali, tunatarajia pia kujenga bandari kavu kama ilivyo Isaka.

“Malampaka pia tutajenga stesheni jengo kubwa lenye mita za mraba 8000 ambayo ndani itakuwa na benki,” maduka na huduma nyingine,” amesema.

Amewataka taasisi mbalimbali kushirikiana na TRC ili utekelezaji wa mradi huo ili usiathiri shughuli mbalimbali za wananchi.

error: Content is protected !!