Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Ujenzi Magomeni kota, Majaliwa atoa maagizo TBA
Habari Mchanganyiko

Ujenzi Magomeni kota, Majaliwa atoa maagizo TBA

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kuhakikisha wanakamilisha kazi iliyosalia ya ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota, Dar es Salaam. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Jumatatu tarehe 20 Aprili 2021, mara baada ya kutembelea mradi huo.

Amesema amefurahi kukuta majengo yamekamilika na kwamba ameridhika na maendeleo ya ujenzi wake.

Majaliwa amesema, Serikali ipo imara na miradi yote ya kimkakati inaendelea kujengwa, hivyo Watanzania waendelee kuwa na imani nayo.

Amesema, Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ipo makini na inaendelea kuwatumikia Watanzania, “tuendelee kuchapa kazi.”

“Siri ya kuwepo mafanikio na maendeleo nchini ni utulivu na amani. Tulianza vizuri tangu Serikali ya Awamu ya kwanza, tutaendelea kuimarisha amani na utulivu,” amesema.

Majaliwa ametumia fursa hiyo, kuwaasa Watanzania watumie muda mwingi kufanya shughuli za maendeleo kuliko mambo mengine yasiyo na tija.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TBA, Daud Kondoro amesema, mradi huo una jumla ya block tano na ambazo zinauwezo wa kuchukua familia 656.

Amesema mbali na ujenzi wa nyumba hizo za makazi, pia katika eneo hilo wanajenga maduka makubwa pamoja na vizimba kwa ajili ya wajasiriamali kufanya biashara.

Mradi ulianza kutekelezwa mwaka 2016 na unatarajiwa kukamilika Mei 2021. Hadi sasa umefikia asilimia 94 ya utekelezaji wake na gharama yake ni Sh.50 bilioni.

Baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makazi za Magomeni Kota, Waziri Mkuu alikagua kituo cha Reli ya Kisasa cha Tanzanite jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!